Zinazobamba

BAADA YA SERIKALI YA JPM KULIFUNGIA GAZETI LA RAIA MWEMA, HASHIM RUNGWE AIBUKA NA KUI "POPOA " SERIKALI,SOMA HAPO KUJUA


NA KAROLI VINSENT
WAKATI ndani ya siku kumi serikali ya Rais ya John Magufuli ikiwa ni teyari imeyafungia magazeti mawili ndiyo naweza kusema baada ya leo serikali kutangaza kulifungia kwa siku 90 gazeti linalotoka mara moja kwa wiki la Raia Mwema kutokana na kuandika habari inayodaiwa inayomchafua Rais Magufuli.

Mbali na Gazeti hilo katika siku hizo, pia serikali hiyo imetangaza kulifungia kwa miaka miwili gazeti la Mwanahalisi kutokana na kuandika habari ambazo serikali inadai zinakiuka kanuni za uandishi wa habari.

Hatua hiyo imepingwa vikali na wanasiasa huku wakisema hatua hiyo ni muendelezo wa serikali ya Rais Magufuli kuminya demokrasia .

Hashim Rungwe (Pichani) ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma ameumbia Mtandao wa Fullhabari.blog, kuwa hatua ya serikali kulifungia gazeti hilo  imekiuka msingi ya haki za binadamu huku akitaja ni mwendelezo wa ukandamizaji wa demokrasia hapa nchini.

“Huu ni muendelezo wa ukandamizaji wa demokrasia,ameaanza kwetu wanasiasa,Leo wanataka kuwatisha wanahabari wasiandike habari  ambazo wa wao hawasipendi,”amesema Rungwe.

Rungwe ambaye alikuwa mgombea wa Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 amesema kwa sasa kinachoonekana kwenye tasnia ya habari ni serikali kujivika koti  Uhariri wa habari.
"Sahivi serikali imekuwa mhariri wa habari,kama utaki watu waandike habari si useme waandike za kukusifia wewe,akumbuke yeye ni baba wafamilia lazima watu wamkosoe,"amesema Rungwe ambaye ni Wakili Msomi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu amesema wameambiwa sababu ya kusitishwa kwa gazeti hilo ni habari hiyo.

Ulimwengu amesema kwa sasa wanashauriana kuona ni nini cha kufanya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo,Dk Hassan Abbasi kwa vyombo vya habari inasema serikali imefikia hatua kulifungia gazeti la Raia Mwema kutokana kuandiika nukuu ya uongo kwa Rais Magufuli.
Amesema toleo la namba 529  la terehe 27 semptemba hadi Oktoba mwaka ilichapisha habari ya Uchambuzi inayosema “URAIS UTAMSHINDI JOHN MAGUFULI”
“Makala  hiyo  ilisheheni  nukuu za kutunga na zisizo za ukweli  zikimsingizia Rais John Magufuli ,Gazeti hili limeonywa sana huko nyuma dhidi ya uandishi wake” Amesema
Kufungiwa kwa Gazeti hili kunakuja ni siku moja baada ya wamiliki wa Gazeti la Mwanahalisi kutangaza kukimbilia Mahakamani kutaka Gazeti hilo lifunguliwe.
    Kufungiwa kwa Gazeti la Raia Mwema linakuwa ni miongozi mwa magazeti zaidi ya 400 kufungia tangia Rais Magufuli aingie madarakani katika miaka yake miwili,
]Magazeti 400 hayo mengi yake yakifungiwa kutokana na kutochapishwa kwa mada mrefu huku yaliobakia yakifungiwa kwa sababu inayotajwa kuwa yanakiuka misingi ya uandishi wahabari. 
TAMKO LA SERIKALI KULIFUNGIA GAZETI LA RAIA MWEMA HILI HAPA.