Zinazobamba

WEMA SEPETU BADO KESI YAKE KIZINGIMKUTI,SOMA HAPO KUJUA


Mrembo Mtanzania Wema Sepetu amekuwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo imekuwa ikiendelea siku hadi siku ambapo leo August 4, 2017 alirudi tena Mahakamani na kilichoendelea ninacho.

Taarifa ikufikie tu kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 4, 2017 imeahirisha kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu na wenzake hadi August 15 na 16, 2017 itakaposikilizwa.