WATUMISHI HOUSING WAPELEKA MRADI WA NYUMBA 500 MKOANI DODOMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Fredy Msemwa akielezea namba walivyojizatiti katika kuiunga mkono serikali uamuzi wa kuhamishia shughuli za serikali katika Mkoa wa Dodoma ikiwa imepanga kuwajengea watumishi nyumba bora na za kisasa Mkoani humo. |
Kampuni hiyo yenye dhamana ya uwekezaji katika nyumba ikiwa ni mpango wa taifa wa makazi kwa watumishi, imeamua kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma na wameshapata eneo la Njedengwa lenye ukubwa wa hekari 55 likiwa limeshapimwa tayari kwa ujenzi wa nyumba 500.
Akielezea mikakati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Fredy Msemwa amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba hizo zitajengwa nyumba 159 na zitakuwa kwa ajili ya watumishi watakaokuwa wamehamia Mkoani Dodoma na wale wanaoishi haoo.
Msemwa amesema, eneo la Njedengwa ni eneo ambalo limeendelezwa tayari likiwa lina huduma zote za kijamii ikiwemo barabara ya lami, maji, umeme na miundo mbinu mingine ambayo inalifanya kuwa eneo bora zaidi kwa makazi ya watumishi na yatai ujenzi umeshaanza na utakamilika baada ya miezi nane (8) na zitakuwa katika mfumo wa aina mbili zile zilizoisha kabisa na zitakazokuwa zimeisha kwa asilimia 80.
Nyumba hizo zitakuwa na mahitaji ya kutosha kabisa kwa watumishi wa umma wa kipato tofauti na utapatikana kwa njia ya mkopo endelevu kupitia benki washirika huku nyumba zilizokamilika kabisa zitauzwa kwa shilingi milioni 56 na zile zilizokamilika kwa asilimia 80 zitakuwa kwa milioni 46 zote zikiwa pamoja na VAT.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Watumishi Housing Raphael Mwabuponde akiwaelezea waandishi wa habari namna ya watumishi kupata nyumba hizo zitakazojengwa katika Mkoa wa Dodoma.
Mbali na hilo, Msemwa amesema wamepokea msaada wa vifaa vya upimaji wa viwanja na miji kutoka benki ya Dunia kwahiyo itarahisisha katika upimaji wa viwanja na pia kuanza kutoa huduma zote za makazi kuanzia uuzaji wa viwanja vilivyopimwa pamoja na nyumba zilizokamilika na huduma hii itaanzia mkoani Dodoma.