WAISLAM NCHINI WAPEWA DARASA TOSHA LA SIKUKU,SHEIKH JALALA ATOA NENO,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Kiongozi wa Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheria Tanzania, Sheikh Hemed Jalala akizungumza na waandishi wa habari kuelekea sikuku ya Eid kesho |
NA KAROLI VINSENT
WAKATI
Waumini wa Dini Kiislam nchini wakiungana na wenzao Duniani kesho wakiwa wanasherekia sikuku ya Eid Haji,Waumini hao wametakiwa kusherekea sikuku hiyo kwa
kuhakikisha wanadumisha amani na upendo katika jamii.
Pia wametakiwa kuhakikisha wanafanya mambo ya
kumpendeza mungu katika sikuku hiyo na kuacha kufanya mambo ya kumchukiza Mungu
.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na
Kiongozi wa Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheria Tanzania, Sheikh Hemed Jalala
wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia sikuku hiyo, ambapo amesema
sikuku hii ni nembo kubwa kwa waislam ,basi hawana budi kuhakikisha wanaijenga
jamii isiyokuwa na aina yoyote ya vurugu.
“Nawaomba waislam tutumie sikuku hii katika
kujitafakari na kuhakikisha tunailinda amani yetu hapa nchini Tanzania ,kwa
kuleta umoja na mshikamano huu kwetu,na tusikubali kufarakana katika
jamii”Amesema Sheikh Jalala.
Kiongozi huyo wa kiroho ameenda mbali kwa kuwataka
waislam kututumia sikuku hii muhimu kwa kusherekea kwa kufanya maasi jambo analodai linakwenda
kinyume na sheria za dini ya kiislam.
“Mtu anayemkosea Mungu Siku ya sikuku ya Eid mtu huyu ni kama
amemkosea mungu siku ya kiama”amesema Shekh Jalala.
Sheikh Jalala pia ameitaka serikali kuhakikisha
wanatumia rasilimali zilizopo hapa katika nchi za Afrika
zitumike katika kutatua tatizo la ajira.
“Bara la Afrika bado linalinasumbuliwa na matatizo
mengi sana ikiwemo umasikini,bado linasumbuliwa na maradhi bado Afrika
inasumbuliwa na njaa,basi tunawaomba viongozi wa Afrika kutumia rasilimali
zilizopo katika maneno yetu zitumike katika kutatua matatizo ya ajira ili
ipatikane jamii yenye kufanya kazi”ameendelea kusema Sheikh Jalala.
Hata
Hivyo,Sheikh Jalala amewataka pia waislam ambao walikwenda kufanya Hija kutumia
njia hiyo katika kuhakikisha wanaijenga jamii nzuri isiyo kuwa na aina yoyote
ya fujo na mfarakano katika jamii.