TECNO NA MAN CITY KUKUZA VIPAJI VYA MPIRA TANZANIA.
Kampuni ya simu ya Tecno Mobile iliyoingia makubaliano ya kibiashara na Timu maarufu inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa miguu nchini Uingereza Klabu ya Manchester City, kwa pamoja wamekuja na mikakati ya kukuza soka nchini Tanzania.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo Bwana Eric Mkomoye, amesema kua pamoja na kuwapo kwa fursa za kibiashara zilizopo kati ya klabu ya Manchester City na Tecno Mobile lakin pia Tecno wamedhamiria kutumia fursa hiyo kukuza viwango vya mpira kwa watoto wa kitanzania ambao wazazi wao pia ni wateja wa kampuni hiyo
“Tutawapa watoto wa kitanzania kadhaa nafasi ya kwenda Manchester city kufanya training kule na pia wakifanya vizuri wanauwezo wa kuchukuliwa kwa academy ya Manchester City , huko watakutana watoto wengine tokea nchi ambazo Tecno Mobile inafanya kazi zake kama Kenya, Uganda, Ghana na Misri na kwa kuanza tutapeleka watoto wawili”
Katika ushirikiano huu pia imeleta simu maalumu itakayotumika alama maalumu ya Tecno Mobile na klabu ya Manchester City, Eric alifafanua.
“Tumeleta Tecno Camon CX Manchester city limited version, ni simu maalumu inayoonesha ushirikiano wetu na Man city pia ni simu maalumu inayotumika wachezaji wa Manchester city katika kupiga picha , hivyo tumeileta sokoni maalumu kwa wateja wetu kipindi waweze kupata experience wanayopata man city katika simu hii.”
Aliongeza “Simu hii inakuja na box kubwa lenye zawadi maalumu kwa wateja kama chupa ya kimichezo, speaker, fimbo maalumu ya kupigia picha pamoja na kava maalumu.”
TECNO Mobile wameleta simu ikiwa ni toleo maalumu la tecno camon cx iliyokua sokoni mapema kidogo ila limeboreshwa Zaidi, hivyo inaenda na wakati uwezo wa kamera yake ni 16mp nyuma na mbele zinazosaidiwa na flashi mbili mbele nanne nyuma, uwezo wake ndani ni 64 GB huku ikisukuma data vizuri kwa 4GB Ram,
Watoto watakaochaguliwa na Tecno Mobile kwenda katika trining hiyo wanatarajiwa kuondoka nchini mwisho wa mwezi nane, na vigezo vikubwa Tecno imetumia wataalamu wa soka nchini kutafuta vipaji hivi, Majina ya watoto hawa yatatangazwa kupitia mitandao ya kijamii ya Tecno Mobile.