Zinazobamba

MGOMO WA TUNDU LISSU NA MAWAKILI NCHI NZIMA LEO WATIKISA,LHRC NAO WAUNGANA KWENYE MGOMO,SOMA HAPO KUJUA





Pichani ni Wanasheria kutoka kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) wakiwa kwenye kuuunga mgomo wa mawakili nchi nzima kupinga tukio la kushambuliwa kwa bomu ofisi ya emma ,

NA KAROLI VINSENT
WAKATI leo na kesho mawakili nchi nzima wakiwa kwenye mgomo wa kutohudhulia  Mahakamani na Mabaraza ili kulaani tukio la kuvamiwa na kulipuliwa na mabomu ofisi ya mawakili wa Imma lililotokea mwishoni mwa wiki.

Mgomo huo umefanyika kwa aina baada ya Kituo cha Sheria na Haki na Binadamu (LHRC) ,Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC)  na mashirika mengine ya TANLAP pamoja na WILDAF ambapo nao wameungana na Chama cha Wanasheria Nchi (TLS) katika kuendeleza mgomo huo.

Hatua ya wao kufanya hivyo wamesema ni kukemea na kulaani tukio hilo ambalo wanadai linahatarisha utetezi wa haki ya uwakilishi na uwezo wa wanasheria kutekeleza majukumu yao. 

Huku wakitekeleza mgomo huo   asasi hizo za binadamu, washirika hao wakiwa wamevaa nguo nyeusi pamoja na kujifunga vitambaa vyeusi mdomoni pamoja na kuwa na mabango yenye ujumbe wa kulaani tukio hilo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutekeleza mgomo huo,Mkurugenzi wa (LHRC)Dkt Helen Bisimba amesema  tukio hilo limeleta hofu katika tasnia ya sheria nchini.

“Tunaungana TLS kulaani tukio hili kwani limeibua hofu kubwa katika tasnia nzima ya sheria ,hususani kwa mawakili,katika kutekeleza  majukumu yao kwa ujumla ,tukio hili ni la kikatili na la kigaidi ambalo linapaswa kukemewa na kupingwa vikali na wadau wote wa haki za binadamu ambapo sisi LHRC tunaungaza na wenzetu kulaani”amesema Bi Bisimba.

Bi Bisimba amendelea kusema kwa uchungu kuwa kwa kipindi cha miaka miwili sasa hapa nchini kumekuwa kukiripotiwa  matukio kadhaa ya kuwashambulia  na kuwatisha wanasheria  pale wanapokuwa wanatekeleza majuku yao .

Ametolea mfano mnamo mwezi Julai mwaka 2016 ,Naibu Mkurugenzi wa  Upelelezi  wa makosa ya Jinai Zanzibar ,Kamishna Msaidizi wa Polisi  Salum Msangi kusema wanasheria wanaotetea wahalifu wataunganishwa na wahalifu katika makosa pamoja tukio lilotokea katika mwaka huo la kukamatwa mwanasheria  LHRC ,Wakili Shilinde Ngulula ambaye alikamatwa na kuwekwa ndani na askari polisi  wilaya ya Ngorongoro wakati akiwa kazini amedai vitendo hivyo ni muendelezo wa ukandamizaji kwa wanasheria.

"Yapo matukio mengi  yanayokanyaga uhuru wa sheria nchini likiwemo lile agizo la Rais John Maguli wakati siku ya sheria 2/2/2017 alipoagiza watuhumiwa wa ujangili kuchukuliwa hatua punde wanapokamatwa,hii ni kauli ya kuingilia mhimili wa mahakama”amesema Bi, Bisimba.

Bi Bisimba ameenda mbali kwa kusema kitendo cha Rais Magufuli kutomteua Jaji mkuu mpaka sasa ,huku akiendelea kumtumia kaimu jaji mkuu ,kitendo hiki ni kinakwenda kinyume na katiba ya nchi na kinashindwa  kuimarisha mhimili wa mahakama na utawala wa sheria nchini.

Pamoja na hayo LHRC wameitaka serikali kupitia jeshi la Polisi nchini kuhakikisha linawakamata watu wote ambao wamehusika katika shambulizi la ofisi ya IMMA na kuhakisha wanachukulia hatua.
Pichani ni Mkurugeni wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)Dkt Helen Bisimba akizungumza na waandishi wa habari leo kuunga mkono mgomo wa mawakili nchini

Aidha,wametaka viongozi wa serikali na vyombo vyake wenye dhamana ya kulinda usalama wa watu nchini na haki za binadamu  kwa ujumla wawajibike au kuwajibishwa  mara moja pale ambapo wameshindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao. 
Rais wa chama cha mawakili nchini (TLS)Tundu Lissu akiwa kwenye Mgomo huo



  TUNDU  LISSU ANENA.
Naye Rais wa TLS,ambaye pia ni Mbunge wa Singida mashariki,Tundu Lissu amesema kwa sasa hali ya nchi kwenye  sheria sio nzuri kutokana kuwepo kwa vitendo mbali mbali.

“Nataka niwambie leo ofisi za Mawakili zinapigwa bomu,leo mwakili wamejaa hofu ,kesho uwenda ikawa zamu ya watu wengini,ndio maana tunapaza sauti zetu kulaani tukio hili”

“Kama yupo leo Wakili ambaye amesusia mgomo wa leo na kwenda mahakamani namuomba afikilie kuwa tukio lile likitokea kwake itakuwaje”amesema Lissu ambaye pia ni Mwanasheria mkuu wa Chadema.
   THRDC wafunguka .
Naye Mkurugenzi wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC),Onesmo Olenguruma amesema kitendo cha kulipuliwa ofisi ya IMMA ni cha kinyama kinatakiwa kupingwa na kila mtu kwani kimeleta hofu katika tasnia ya sheria nchini.
   HALI YA MAHAKAMA IPOJE
Fullhabari.blog ilifika kwenye mahakama mbali mbali jijini Dar es Salaam na kushudia idadi ya mawakili wengi wakiwa wameungana na TLS katika kutekeleza mgomo wa kulaani tukio hilo.
Akizungumza kwa sharti la kutotaja jina lake,wakili mmoja maarufu alisema lazima naye alishiriki kwenye mgomo huo kwani kitendo walichofanyiwa wenzao ni cha kinyama.
“Tunakwenda kubaya sana lazima wanasheria tuungane kulaani hali hii,huu mgumo ni wa kila mtu,maana leo tumeona ndani nchi yetu mihili aiheshimiwi kabisa ,Mahakama hazipo huru ambalo ni jambo la hatari kabisa katika nchini lazima tuungane kupiga vita”amesema Wakili huyo msomi.