KITUO CHA UWEKEZAJI WASAJILI MIRADI 209 ,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni ni Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC)Geofrey Mwambe akizungumza na waandiishi wa habari (Hawapo pichani )kuhusu miradi iliyotekelezwa na kituo hicho tangu kuanza kwa mwaka huu |
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TIC Geofrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari, alisema kiwango hicho ni kikubwa ukilinganisha na mwaka uliopita ambapo walisajili miradi 306 tu.
“Hadi sasa tumekwisha sajili miradi 209 kwa kipindi cha miezi saba, hii inamana kwamba tunaeza kusajili miradi mingi zaidi kwa muda huu uliobaki kabla ya mwaka huu kumalizika,” alisema Mwambe.
Aidha alisema wameandaa mpango maalum wa Mfuko wa Benki ya Ardhi ambao utasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa ardhi na kuleta ufanisi katika upatikanaji wa maeneo ya ujenzi wa viwanda pamoja na uwekezaji mwingine.
Sehemu ya Waandishi wa habari wakisikiliza mkutano huo, |
Alisema hadi sasa maeneo yaliyopatikana kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ni Kigamboni na Tanga na wanategemea kuongezeka kwa mitaji ya kutoka nje na ndani yaani FDI na DD1 kutokana na kupata miradi mikubwa Sita.
Mwambe alifafanua kuwa miradi hiyo yenye hadhi ya kimkakati iliyosajiliwa na TIC na kupitishwa na Baraza la Taifa la uwekezaji. alisema miradi hiyo kwa pamoja inategemewa kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani sh. bilioni 2.626 na inatarajiwa kuzalisha kiasi cha ajira 13,885 ambazo zitanufaisha watanzania.
alieleza kuwa juhudi za uhamasishaji ujenzi wa viwanda zimeweza kuzaa matunda na mpaka sasa wameweza kusajili viwanda vikubwa ambavyo vitasaidia katika kubadilisha hali ya uchumi wa nchi.