Zinazobamba

HII NI BALAA SASA USAHILI WA NAFASI ZA KAZI TRA HAIJAPATA KUTOKEA,NI UMATI MKUBWA,KAULI YA LOWASSA YAANZA KUTIMIA

Maelfu ya vijana wakigombania kuingia mlangoni wakati wa usahili wa nafasi za kazi zilizotangazwa na mamlaka ya Mapato nchini (TRA)
KILE kinachoonekana kuwa kauli aliyoitoa  Waziri Mkuu wa Zamani,Edward Lowassa  kuwa  vijana ambao hawana kazi ni bomu linalosubili kulipuka,ni kama kauli yake inaanza kutimia.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Kauli hiyo imejipambanua leo wakati wa Usahili wa nafasi za kazi zilizotangazwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambazo zimeshtua watu wengi kutokana na kushuhudiwa umati mkubwa watu wakiziwania nafasi hizo jambo linalonesha kuwa suala la  ajira ni gumu nchini kuriko kupindi chote cha nchi tangia kupata uhuru.
Uchunguzi uliofanywa kwa kina na Fullhabari.blog umebaini kati ya nafasi 400 zilitangazwa na Mamlaka hiyo ,watu walijitokeza kwenye usahili huo wanafikia zaidi ya elfu 20.

Usahili huo ambao ulikuwa unafanyika kwa kanda mbali mbali unatajwa ndio usahili ambao umeshudia watu wengi kujaa huku nafasi zilizotangazwa ni chache.

Akizungumza na Fullhabari.blog kwa sharti la kutotaja jina lake mtandaoni,Ofisa mwandamizi kutoka tume ya sekretaliti ya Ajira nchi ambayo ndio imepewa jukumu la kutangaza na kuajiri nafasi mbali mbali ndani ya serikali amekiri
 kuwa hali ya sasa ni mbaya sana kutokana na kuwepo na idadi kubwa ya watu wanaotaka ajira.

"Sikufichi hali ya nchi sasa ni mbaya,watu wengi wanamaliza chuo kikuu ni wengi sana,unaona nafasi 400 wanaotaka TRA  huwezi amini watu waliomba ni zaidi ya 56500 sema kwa kulinda gharama za kufanya usahili tumeamua kuwapunguza kwa kuangalia makosa madogo “amesema Ofisa huyo,
.
Amesema katika watu hao elfu 56500 walikuwa na sifa stahiki kwenye elimu ikiwemo kuwa na shahada moja na kuendelea ila wameamua kuwapunguza kwa kuangalia makosa modogo ikiwemo kama mwombaji ameshindwa kuweka mhuli wa wakili katika maombi yake ya kazi .

Akizungumzia hali hiyo,Mchambuzi wa masuala mbalimbali nchini kutoka chuo kikuu huria n,Bilal Soud amesema kama watawala wasipotafuta njia ya kutatua hali ya ukosefu wa ajira wajue huko mbeleni taifa litakuwa gumu kutawalika.

“Kuna siku watanzania mtakuja mkumbuka Lowassa,wakati yupo CCM alitabili haya watu wakambeza,maana hali ni mbaya sana leo mwenyewe umeshudia tangia utawala huu uingie madarakani makampuni mengi yamekufa,mengi yamepunguza watu kutokana na sera mbovu ,na vijana wanamaliza vyuo vikuu ni wengi matokeo yake ni haya,na asikwambia mtu hata hizo nchi zenye machafuko duniani suala la ajira linachangia”

“Leo mtu  kasoma hana ajira,leo hii serikali yenyewe imeshindwa hata kuweka mazingira mazuri ya vijana kujiajiri ikiwemo hata kumkopesha mitaji,matokeo yake ni haya ,tunakwenda kibaya ndugu Mwandishi’amesema Soud.