FREEMAN MBOWE AISHTUA SERIKALI YA JPM,YAIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
HATIMAYE hoja zilizotolewa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zimemuibua msemaji wa serikali wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Hassan Abbas, anaandika Catherine Kayombo.
Abbas ameibuka leo mchana na kusisitiza kwamba uchumi wa Tanzania bado uko imara tofauti na ilivyosemwa na Chadema kupitia mwenyekiti wake Freeman Mbowe, alipokutana na wanahabari kueleza maazimio ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichofanyika tarehe 29-30 Julai jijini Dar es Salaam.
Mbowe aliyataja maeneo yanayoyumbisha uchumi wa nchi kuwa ni pamoja na mwenendo wa mikopo katika sekta binafsi, ongezeko la deni la taifa na kushuka kwa mzunguko wa fedha kusababisha kuathiri biashara.
Akizungumza na wanahabari, Abbas amesema, uchumi wa upo vizuri ukilinganisha mataifa mengine barani Afrika, kwa miaka mitatu mfululizo bado uko katika ukuaji usiopungua asilimia 7.0 hadi 7.2.
Amesema ukuaji wa uchumi unaizidi Rwanda ambayo inakua kwa 6%, Uganda 5% na Kenya 6.4%.
Amesisitiza kuwa uimara wa uchumi wa nchi ni namna ya kudhibitiwa kwa mfumuko wa bei, kuendelea kuvutia uwekezaji na utekelezaji wa miradi mikubwa.
Amewataka wananchi kuchapa kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo bila kutegemea nguvu ya serikali.