Zinazobamba

CHADEMA WAANZA KUISAKA HAKI YA DHAMANA,SOMA HAPO KUJUA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeandika barua kwa ofisi ya Jaji Mkuu wa Tanzania, kikiomba wafuasi wao wanapokamatwa kwa makosa yanayodhaminika waweze kupewa dhamana, anaandika Irene David.
Ofisi hiyo kwa sasa inaoongozwa na Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, ambaye anakaimu.
Hayo yamesemwa leo na Makamu Mwenyekiti Taifa wa chama hicho (Bara), Profesa Abdallah Saffari, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Makao makuu jijini Dar es Salaam.
Saffari amesema kuwa ametaka baadhi ya mahakimu kutenda kazi zao kwa kufuata sheria wakati wa kutoa hukumu hasa kwa kesi zinazowakabili wapinzani.
Ametoa mifano ya baadhi ya viongozi hao akiwemo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alifikishwa mahakamani kwa kosa la uchochezi na mshtakiwa alinyimwa dhamana.
Wengine walionyimwa dhamana ni pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini , Godbless Lema na hivyo kulazimika kukaa rumande kwa zaidi ya miezi mmine.
“ Pia wajumbe wa serikali ya mtaa ambao pia ni wanachama wa chadema, 24 julai 2017 walinyimwa dhamana .” amesema Saffari.
Profesa Saffari amesema Chadema haitavumilia uonevu huo unaofanywa na baadhi ya Mahakimu na kuwataka kufuata sheria zitokanazo na misingi ya katiba