Zinazobamba

WIZARA YA NISHARTI NA MADINI YAFANYA MABADILIKO MAKUBWA SHERIA YA MADINI,SOMA HAPO KUJUA

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia).
mwaka 2010

Wizara ya Nishati na Madini imefanya mabadiliko ya Sheria ya Madini kwa kuongeza malipo ya mrabaha kutoka asilimia 4 hadi 6 kwa madini ya Metali (dhahabu, shaba na fedha) ambapo mabadiliko hayo yametokana na marekebisho ya sheria ya madini ya

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mabadiliko hayo na kusema kila anayetaka kusafirisha madini lazima yakaguliwe pamoja na kuthaminishwa kabla kuondoka katika ardhi ya Tanzania.

"Kupitia marekebisho ya sheria za fedha na sheria ya kodi, hivi sasa kila mtu au kampuni anayetaka kusafirisha madini nje yatakaguliwa na kuthaminishwa na atalipa ada ya ukaguzi ambayo ni asilimia 1 ya thamani ya madini anayosafirisha. Pia mchimbaji mdogo anayeuza madini kwa 'Broker au kwa 'Dealer' atakatwa asilimia 5 ya thamani ya madini kama 'with holding tax' ambayo itakusanywa na 'Broker' au 'Dealer' na kupelekwa TRA",amesema Prof. Mdoe.

Pamoja na hayo, Prof. Mdoe amesema katika kipindi hiki cha mpito serikali imesimamisha utoaji wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini mpaka pale Tume itakapoundwa na kuanza kazi yake rasmi japokuwa kwa sasa shughuli zote zitafanyika chini ya usimamizi wa Kamishna wa Madini.

Kwa upande mwingine, Prof. Mdoe amesema kufutwa kwa TMAA na ofisi za madini za kanda, watumishi waliyokuwa wanafanya kazi kwenye Taasisi au Ofisi hizo ambao hawana tuhuma zozote wataendelea na ajira zao kama kawaida kwa sababu ni watumishi wa serikali katika Wizara ya Nishati na Madini.