WAZIRI MAKAMBA AIBEBESHA ZIGO NEMC
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira mh january makamba ameliagiza baraza la taifa la usimamizi wa mazingira kuhakikisha wanaziondoa gereji zote bubu zilizopo pembezoni mwa mtaro wa bungoni uliopo ilala jijini dar es salaam.
Mh makamba ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa ukuta na mitaro kwa ajili ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo ametoa wiki mbili kwa nemc kuhakikisha wanaziondoa gereji bubu katika eneo hilo.
“Tumekuja kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo na kandokando ya mto tumekuta mazingira sio mazuri hivyo endapo shughuli hizo zitaendea kufanyika zita athiri mwendelezo wa utekeleza wa mradi hivyo nemc kwa kushirikiana na taasisi zingine kuhakikisha gereji hizo zinatoka kwa muda uliopangwa”
Aidha mh makamba amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni sehemu ya malaengo ya wizara ya kuboresha hali ya mazingira nchini na kwamba miradi kama hiyo inatekelzwa nchi zima.
Mhandisi frank juvenasy kutoka kampuni ya dezo civil contracter ambao ni wa wasimamiz wa mradi wa ujenzi wa ukuta katika ufukwe za chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere cha jijini dar es salaam amesema kampuni hiyo inatalajia kumaliza ujenzi wa ukuta huo kabla ya mwisho mwa mwezi wa nane na mwezi wa tisa kukabidhi.
“Asilimia kubwa na ujenzi tumesha malinza kama mnavyoona tumesha unganisha kuta zote na kazi iliyobaki kwa sasa sio kubwa hivyo hadi mwezi wa tisa tutakabidhi ujenzi wa mradi huo”
Katika ziara hiyo mh makamba alitembelea mradi wa ujenzi wa mtaro wa bungoni, ujenzi wa ukuta kigamboni chuo cha kumbukumbu ya mwl nyere na kuhitimisha kwa kutembelea ujenzi wa ukuta wa barabara ya obama uliopo jijini dar es salaam.