PBPA YASEMA MELI 7 KULETA MAFUTA YA MWEZI WA TISA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
Lumato amebainisha kuwa kwa sasa mahitaji ya mafuta yameongezeka kutokana na wafanyabishara kuridhishwa na bajeti ya serikali 2017-2018 iliyopitishwa na Bunge.
WAKALA wa Uigizaji Mafuta kutoka nje ya nchini (PBPA) wamesema takribani meli 7 zinatarajia kuingiza mafuta nchini kwa ajili ya matumizi ya mwezi wa tisa.
Pia,(PBPA) imesema wafanyabiashara wa mafuta nchini wameridhishwa na Bajeti ya serikali ya mwaka 2017-2018 kutokana na kutoa fursa ya kuyarusu magali mengi kuingia barabarani jambo wanalodai litapelekea matumizi ya mafuta kuongezeka.
Hayo yameelezwa leo Jijini dare s Salaam,na Kaimu Mkurugenzi wa (PBPA),Modestus Lumato wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kuitangaza kampuni ambayo iliyoshinda tenda ya kuagiza mafuta toka nje ya nchini.,
Amesema kati ya hizo meli hizo, meli tatu zitakuwa na mafuta ya Diseli,tatu zikiwa na mafuta ya Petroli huko moja ikiwa ni mafuta Taa.
Amesema kwa sasa zimejitokeza kampuni 7 kwenye kuwania tenda ya uigizaji mafuta hayo kuyaleta hapa nchini huku ikitakiwa kampuni moja .
Lumato amebainisha kuwa kwa sasa mahitaji ya mafuta yameongezeka kutokana na wafanyabishara kuridhishwa na bajeti ya serikali 2017-2018 iliyopitishwa na Bunge.
‘‘kwenye mwezi wa sita wafanyabiashara walipunguza wingi wa uigizaji wa mafuta kutokana na kusubiri bajeti ya serikali,lakini kwa sasa bajeti imepita na imetoa ruhusa kwa magari mengi kuingia barabarani kwa kutoa tozo za kodi zilizokuwa zinazuia magari kuingia barabarani ,kwa sasa magari mengi yataingia barabarani na kupelekea mafuta mengi kutumika”amesema Lumato.