VIGOGO WA CHADEMA WAENDELEA KUJAZANA MAGEREZANI,SOMA HAPO KUJUA
MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga imewahukumua viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko usio halali, anaandika Mwandishi Wetu.
Waliohukumiwa kwenda jela ni aliyekuwa Diwani wa Kata ya Igunga ambaye kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Igunga, Vicent Kamanga (52), Mwenyekiti wa Chadema Tawi la Mwamsunga, Fea Rifa (41) na Katibu wa Chadema Tawi la Mwamsunga katika Kijiji cha Mgongoro, Luhanya Zogoma(48).
Taarifa zaidi zitakujia kwa kadri tunavyopokea kutoka wilayani Igunga, Tabora.