Zinazobamba

TUNDU LISSU KUCHEZA KARATA KESHO,SOMA HAPO KUJUA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, itaamua Dhamana ya Rais wa Chama Cha Wanasheria nhini (TLS) Tundu Lissu.

Uamuzi huo unatokana na Pingamizi la Dhamana liliwasilishwa Mahakamani hapo Juzi na Jopo la Mawakikli wa Serikali.

Mawakili wa Serikali waliibua  Mahakamani hapo hoja ya kuzuiliwa kwa dhamana ya Lissu kutokana na kushtakiwa na makosa ya uchochezi zaidi ya nne Mahakamani.

Jopo la Mawakili wa Utetezi  lipinga hoja hizo  kwa kudai kwamba Dhamana ni haki ya Mshtakiwa na kwamba Mashtaka ya Lissu yanadhaminika.