TGNP BADO WALIA NA UKATILI WA KIJINSIA
Wanaharakati kutoka mtandao wa kijinsia wa TGNP waguswa na ukatili wa kijinsia unaofanyika katika jamii na kuamua kuifanya kuwa agenda kuu kuelekea tamasha la jinsia.
Afisa Program wa Harakati na ujenzi wa pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Anna Sangai akitoa mawasilisho kwenye Semina iliyofanyika mapema jana kwenye ofisi za mtandao wa jinsia jijini Dar es salaam |
Wakijadiliana jana ndani ya ukumbi wa mtandao huo mabibo jijini Dar es salaam, wanaharakati wamekubaliana kubeba dhana hio ya ukatili wa kijinsia maana wanaamini ukatili unaathiri maeneo mengi yakiwemo ya afya, elimu, jamii na uchumi hali inayopelekea kudidimiza ustawi wa maendeleo kwa mwanamke.
Baadhi ya wanaharakati wakiwa makini kusikiliza Semina iliyofanyika mapema jana ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam |
Aidha,Wanaharakati hao wamekubaliana kutumia njia mbali mbali za kisanaa zikiwemo za ushahiri, ngonjera, maigizo na matumizi ya mabango na picha zenye michoro inayoelimisha watu kuhusiana na upingwaji wa ukatili wa kijinsia katika jamii.
Baadhi ya wanaharakati wakifuatilia Semina iliyofanyika ofisi za Mtandao wa Jinsia(TGNP) Mabibo Dar es salaam |