Zinazobamba

Taarifa ya serikali kuhusu watumishi waliokata rufaa ya vyeti feki

WATUMISHI WA UMMA WALIOKATA RUFAA KUHUSU UHALALI WA VYETI

Watumishi wa umma waliowasilisha vyeti vyao vya kuhitimu kidato cha nne, cha sita na ualimu kwa ajili ya rufaa katika Baraza la Mitihani la Taifa (NETA) kuhusu zoezi la uhakiki, wanatakiwa kuwasiliana na waajiri wao ili kupewa matokeo ya hatma ya rufaa kuhusu uhalali wa vyeti vyao.

Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao mbalimbali ikiwa ni majina ya wanaodaiwa kuwa watumishi wa umma na maeneo yao ya kazi ikiwa na kinachodaiwa matokeo ya rufaa zilizokatwa kuhusu uhalali wa vyeti vya elimu kwa wahusika. Wananchi na watumishi wote wanaelezwa kuwa, serikali inao utaratibu rasmi wa kutoa taarifa na mawasiliano.

Taarifa inayosambazwa haijatolewa na serikali na ipuuzwe.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali,

Ofisi ya Rais-Utumishi,

08.07.2017