NGOME ya Vijana ya chama cha ACT-Wazalendo, imesema kuna hatari ya utawala
wa sheria nchini kuporomoka endapo watanzania hawatapigania sheria na amani ya
nchi, anaandika Hamisi Mguta.
Hayo yameelezwa leo na Karama Kaila, Mwenezi wa Ngome ya Vijana ya chama
hicho, katika tamko lao ikiwa ni siku nne tangu kukamatwa kwa Halima Mdee,
Mbunge wa Kawe (Chadema) kwa amri ya Ally Hapi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
(DC).
“Tukumbuke kuwa wazee wetu waliopigania uhuru
wa nchi hii hawakufanya hivyo kumuondoa mtu mwenye ngozi nyeupe, bali walifanya
hivyo wakitarajia kuondoa kila aina ya uonevu dhidi yao ikiwemo kubanwa kwa
uhuru wa kujieleza na kujiamulia mambo yao bila kuvunja sheria,” amesema Kaila.
DC Hapi aliagiza Mdee akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa 48 Julai 4 kwa
kudai kuwa alitoa maneno ya kukashifu na ya uchochezi katika mkutano wake wa
Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) uliofanyika Julai 3 makao makuu ya chama
hicho alipozungumza kuhusu msimamo wao kwa wanafunzi waliopata mimba kurudi
shuleni.
Kaila amesema baadhi ya wateule wa rais wamegeuza kauli mbalimbali kutoka
kwa rais kama sehemu ya kuwakomoa wenye mawazo tofauti na kauli au matakwa ya
rais, huku akisisitiza kuwa misingi ya utawala bora ni kuheshimu katiba ya nchi
ambayo ndiyo sheria mama.
“Amri ya mkuu wa wilaya ya kinondoni kuamuru kukamatwa na kuwekwa kizuizini
kwa mbunge wa Kawe ni matumizi mabaya ya sheria na uvunjifu wa katiba ya nchi
ambayo viongozi wa umma wameapa kuilinda na kuisimamia.
“Tunasema hivi kwa sababu Mdee hakumtukana rais wala hajatoa maneno yoyote
yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kama anavyodai DC Alli Hapi,” amesema
Kaila
CHAMA CHA ACT-WAZALENDO CHAJITOSA SAKATA LA KUKAMATWA MDEE,WAIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
15:28:00
Rating: 5