SAA CHACHE BAADA YA KUPITISHWA KWA SHERIA MPYA YA MAKINIKIA… ACACIA YAKIMBILIA KORTINI
Saa chache baada ya bunge kipitisha sheria ya marekenisho ya sheria mbalimbali itayayoleta mageuzi makubwa katika usimamizi wa rasilimali za taifa, kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imemtaarifu msuluhishi kuhusu uwepo wa mgogoro kati yake na serikali ya Tanzania.
Serikali iliwasilisha bungeni miswada mitatu inayohusu rasilimali za taifa ambayo ina lengo la kubadili sheria zinazosimamia madini sasa nchini kufuatia kubainika kuwa taifa linapoteza mabilioni ya fedha kila mwaka kupitia sekta ya madini.
Baadhi ya mapinduzi yatakayoletwa na sheria hizo ni pamoja na Benki Kuu ya Tanzania kupewa mamlaka ya kuhifadhi dhahabu baada ya kutokufanya hivyo kwa miaka mingi, huku sheria ikitamka kuwa madini ni mali ya watanzania wote kupitia kwa rais wa nchi.
Sheria hizo zitaiwezesha serikali kufanya uangalizi wa maeneo ya uchimbaji wa madini huku ikihakikisha hakuna ndege itakayotua na kuondoka na madini kama ilivyokuwa awali.
Kufuatia mabadiliko hayo, Acacia jana ilitoa taarifa kuwa Kampuni ya Bulyanhulu Gold Mine (BGM) na Pangea Mineral Limited (PML) zimetoa notisi ya usuluhishi kufuatia uzuiwaji wa usafirishaji wa mchanga wa madini.
Taarifa hiyo iliyochapishwa katika tovuti rasmi ya Acacia ilieleza kuwa, notisi hizo zinarejea mgogoro wa sasa na serikali ya Tanzania dhidi ya BGM NA PML kwenda katika usuluhishi.
Japo kuwa Acacia hawakueleza wamefungua wapi amombi hayo ya usuluhishi lakini walieleza kufanya hivyo kwa wakati huu ni jambo muhimu ili kulinda kampuni wakaeleza pia majadiliano ndio njia bora itakayosaidia kuleta maafikiano ambapo wakati huo wote wao wateendelea kufanya kazi Tanzania.
Wakati majadiliano ya usuluhisi yatakapoanza, Acacia hawatakuwa sehemu ya majadiliano hayo yatakayofanyika kati ya Tanzania na Barrick Gold ambao ndio wamiliki wakubwa wa Acacia.
Aidha wamesema kuwa maafikiano yoyote yatakayofikiwa katika majadiliano hayo yatatakiwa kuridhiwa na Acacia na kwamba watatoa ushirikiano kwa Barrick wakati wa mazungumzo.
Acacia walisema kuwa mgodi yake mitatu inaendelea na uchimbaji kwa kutumia makubaliano ya awali na kwamba itaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu yatakayojiri pamoja na miswada iliyopitishwa na bunge la Tanzania.