RAIS MAGUFULI ATISHIA KUIFUNGA MIGODI YA MADINI,SOMA HAPO KUJUA
Rais Dkt. Pombe Magufuli amesema atachukua uamuzi wa kufunga migodi yote iliyo chini ya wawekezaji ambao amewaita kuzungumza nao kutokana na kubainika wizi katika Makinikia ya mchanga yaliyokuwa yakitoka katika migodi hiyo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 50 kutoka Kibondo mpaka Nyakanazi Mkoani Kigoma ambapo amesema ni bora migodi hiyo ikagaiwa kwa watanzania ambao wanachimba na kulipa kodi kuliko kuwapa wawekezaji ambao hawalipo kodi pamoja na kuibia nchi.
"Ni mara kumi migodi igawanywe kwa watanzania, wachimbe wenyewe tupate kodi kuliko hao wanaojiita wawekezaji, hawalipi kodi. Kama wawekezaji hao wangefuata utaratibu unaotakiwa ikiwemo ulipaji wa kodi ingesaidia kufanya maendeleo mengi nchini kwa kuboresha huduma zote za kijamii ikiwemo elimu na afya. Niwatake wananchi tusimamie kwa pamoja katika hili ili tuweze kutetea maslahi ya nchi yetu", amesema Rais Magufuli.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa awe mkali na kuchukua hatua kwa makandarasi wote waliopewa tenda endapo watabainika kufanya kazi hovyo hovyo na pole pole jambo ambalo litakwamisha kukamilisha kwa miradi ya maendeleo kwa haraka hasa barabara.
RAIS MAGUFULI ATISHIA KUIFUNGA MIGODI YA MADINI,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
19:36:00
Rating: 5