RAIS MAGUFULI AAPA KUFUKUZA KAZI MWALIMU ATAKAYEFANYA HIVI,SOMA HAPO KUJUA
Rais John Magufuli amesema mwalimu mkuu atakayeruhusu mwanafunzi aliyejifungua kurudi shuleni kuendelea na masomo katika shule za Serikali, atafukuzwa kazi.
Rais ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 4) alipokuwa akihutubia wananchi wakati akizindua mradi wa maji Sengerema.
“Ni ukweli pia kuwa wanafunzi waliopata mimba hawarudishwi shuleni, kuna ujanja ujanja wa walimu, wanaandika cheti kuwa alikuwa amelazwa,” amesema na kuongeza:
“Nikimuona Headmaster, amerudisha mwanafunzi aliyepata mimba, kwenye shule za Serikali, yule mwalimu anaondoka.”
Rais amehoji: “Wote waliopata mimba wamebakwa?” Alihoji na kuendelea, “wanafanya mambo haya kwenye picha, wakipata mimba kwa namna hiyo arudi shule.”
Ameongeza: “Niwaombe wazazi wawachunge watoto, hizi mimba zinatokana na wazazi wetu ni lazima wazazi tujifunze kulea, tumechagua kueleza ukweli, tuambiane ukweli.”