MBUNGE HUYU WA UKAWA ALAZWA SERO,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea yuko rumande tangu jana baada ya kukamatwa na Polisi akituhumiwa kuendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda.
Akithibitisha kukamatwa kwake leo Alhamis Julai 20, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Mrosso amesema mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni.
Amesema amekamatwa na askari wa usalama barabarani Temeke akiendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda wake.
“Askari wa usalama barabarani walipomhoji aliamua kuwapuuza na kuondoka zake,” amesema.
Amesema polisi walimfuatilia na kumkamata na sasa anaendelea kuhojiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.
“Atafikishwa mahakamani kama tunavyofanya kwa raia yoyote, nafasi yake kama mbunge haiwezi kuwa sababu ya kutofuata sheria,” amesema.