Zinazobamba

Maambukizi ya VVU yapiga kambi kwa wanandoa

WATU waliofunga ndoa na kuunganika kuwa kama mwili mmoja na kuepukana na masuala ya kufanya ngono zembe, imebainishwa wao kwa sasa ndio wamekuwa vinara wa kupata maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), kutokana na kutozingatia sheria na kanuni za ndoa, ananadika Mwandishi Wetu.
Imeelezwa kuwa watu wamekuwa wakiingia kwenye ndoa kama fasheni, bila ya kufahamu nini maana ya kufunga pingu hizo za maisha, na kujikuta baada ya muda mfupi wamechokana na kuanza kufarakana.
Hayo yalizungumzwa juzi na mwandishi wa kitabu cha Sakramenti ya ndoa katika nyumba aminifu Paschal Maziku, wakati akikitambulisha kwa waumini wa Kanisa Katoliki mjini Shinyanga.
“Tulifanya utafiti na kugundua wanandoa ndio wamekuwa vinara wa maambukizi mapya ya VVU, ambapo kisheria wanandoa ndio wanapaswa kuwa salama sababu kabla ya kufunga pingu za maisha huwa wanapimwa afya zao, lakini kwa hali ya sasa imebadilika na wengi wao ndio
waathirika wa Ukimwi,” amesema Maziku