Zinazobamba

LISSU ASEMA ''ANAYEBISHA RAIS MAGUFULI SIYO DIKTETA HANA AKILI TIMAMU",SOMA HAPO KUJUA

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amezidi kusisitiza kuwa Rais John Magufuli ni dikteta na anayebisha hana akili timamu, anaandika Irene Emmanuel.
Hii ni mara ya pili kwa Lissu kumwita Rais Magufuli kuwa ni dikteta, awali alisema ‘Rais Magufuli ni dikteta uchwara na anastahili kupingwa’, kauli hiyo ilisababisha kufunguliwa kesi kabla ya kufutwa.
“Juni 29, mwaka jana nilisema kwamba, dikteta uchwara huyu anastahili kupingwa na kila mtanzania mwenye akili timamu,” amesema Lissu.
Lissu aliongeza: “Kwamba leo tukisema, utawala wa rais Magufuli ni utawala wa kidikteta wanaoweza kubisha ni wale wanaokula meza moja au wasiokuwa na akili timamu.”
Amesema siasa zinazoendelea sasa nchini, siyo za vyama vingi kwani ni upendeleo mkubwa, chama tawala ndiyo chenye ruhusa ya kufanya siasa na wanapofanya wapinzani wanaonekana waharifu, huu ndiyo udikteta.
“Leo hii, hakuna chama kinachofanya mikutano au maandamano isipokuwa CCM, namimi sijawahi kuona, au kusikia mahali popote kwamba CCM wametoa taarifa ya mkutano,” amesema Lissu.
Lissu amesema nchi nzima hofu imetanda kwa vyombo vya habari, vyama vya siasa mpaka kwa wananchi, lakini na uwepo wa hofu, Rais amevuruga utumishi wa umma kwa kufukuza watumishi bila kufuata utaratibu uliopo katika sheria za utumishi.
Aidha, Lissu amewasihi wananchi kupaza sauti zao kila mmoja kwa nafasi aliyokuwa nayo ili kuiondoa nchi katika utawala wa kidikteta, kinyume na hapo Taifa litazidi kuelekea kubaya.