Zinazobamba

HUU NDIO UGEUGEU WA ZITTO KABWE,SOMA HAPO KUJUA

ZIARA ya Rais John Magufuli mkoani Kigoma, imethibitisha kuwa Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) ni kigeugeu, anayeweza kubadili kauli yake wakati wowote ili kukidhi mipango yake – haaminiki, anaandika Mwandishi Wetu.
Katika mkutano wa hadhara wa Rais Magufuli hadhara uliofanyika Kigoma mjini jana,
 Zitto ambaye alifukuzwa unachama chadema na kwenda kuanzisha kinachoitwa na kuitwa Chama cha Upinzani ,ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kazi nzuri inayofanya huku akisema kuwa Rais Magufuli ameonesha njia kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji.
“Mheshimiwa Rais hii ndiyo Kigoma, na watu wa Kigoma wanakukaribisha na wanakupenda sana kwasababu ya maendeleo. Tunakushukuru sana leo kwa uzinduzi wa mradi wa maji ambao utamaliza kabisa tatizo la maji katika mji wetu,” alisema Zitto.
Wakati Zitto akisema hayo leo, awali alitumia ukurasa wake Twitter kueleza kuwa ziara za Rais zinazofanyika ni usanii na kwamba hakuna mradi wowote mpya wa maendeleo uliopo mkoani Kigoma na kanda ya Magharibi kiujumla.
“Kuzifungua (barabara) ni usanii tu. Hakuna mradi mpya kanda ya Magharibi tangu Novemba 2015. Ni kuwahadaa wananchi tu na serikali inajua,” aliandika Zitto.
Hata hivyo, tofauti na ilivyotarajiwa katika mkutano wa jana Zitto ameishia kumpongeza Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kwa uzinduzi wa mradi wa maji ambao umeanza 2013 na ulitakiwa kuisha mwaka 2015.
Zitto ameshiriki na kupongeza uzinduzi wa miradi ambayo hapo awali alisema ni ya “usanii tu” na yenye lengo la “kuhadaa wananchi.”

TUMFAHAMU ZITTO KABWE NA UGEUGEU WAKE

Zitto Kabwe nimetokea kumfuatilia tangu alipokuwa Mbunge mwaka 2005 hadi 2015,nimegundua Mbunge huyu amekuwa kama mtu aliyekufa ambaye anataka kufufuka kwa jamii.
Miaka miwili iliyopita kiongozi huyo wa Act –wazelendo alihitisha mkutano mkubwa wa Hadhala pale Mwembe Yanga Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam pamoja na Mambo mengine mkutano ule ambao ulikuwa ukirushwa moja kwa moja na Baadhi ya Televisheni pampja na Redio chache,ulinadiwa na viongozi wa chama Cha ACT.
Viongozi hao walikuwa wakitumia njia mbali mbali ikiwemo Magazetipamoja na Mitandao ya Kijamii wakitumia njia hiyo kuwatangania wajitokeze kwenye uwanja huo kwa Madai kiongozi wao wa ACT-Wazalendo anatayataja Majina ya Watanzania walioficha Pesa Uswisi.
Naweza kusema katika watu nilioshawishika hata mimi mweyewe,kwakuwa nakumbuka miaki ya nyuma Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelea Chadema Dokta Wilbroad Slaa alitumia uwanja huo wa Mwembe Yanga kutaja Mafisadi “Papa” kumi na kweli Katibu huyo wa Chadema aliwataja.
Lakini hata Viongozi wa Act-Wazalendo nao walitumia njia hiyo hiyo ya Dakta Slaa kwa kusema nao watataja majina ya watanzania hao ambazo Zitto kabwe anawaita ni “Vigogo”.
Mwisho wa Siku watanzania wakajitokeza kwa wingi kwenye Uwanja huo wakisubuli kile kilichokuwa kinasemwa na Zitto kabwe kuwataja walioficha Mabilioni ya Uswisi.
Mpaka inafika saa kumi na mbili na nusu kiongozi huyo wa Act alishindwa kuwataja Vigogo hao zaidi ya kusema
“Nawataja walioficha pesa Uswisi,nawaambieni tena ni wamiliki wa Makampuni mbali mbali hapa nchini ila kutokana na sheria zilivyo mtayapata kwenye vyombo vya Habari kesho”ndivyo alivyosema Zitto.
Licha ya kusema vivyo viongozi wa ACT walikuwa wakiwapa waandishi wa Habari kile wanachodai ni watanzania walioficha pesa  nchini Uswisi,lakini ukishudia majina takribani tisini na tisa yote yametawaliwa na watu wenye asili ya India.
Hapo ndipo nikapata Mshtuku juu ya mwanasiasa huyo,je alilokuwa analinadi takribani miaka zaidi ya kumi ndani ya Bunge na hata nje kuwa ninamajina wa watanzania wanaoficha Pesa Uswisi ndio hawa wahindi?
Hivi siku zote amekuwa akisema mbele ya waandishi wa Habari kwamba kuna Wakuu wa Jeshi wastaafu pamoja na Mawaziri wa Zamani pamoja wa wabunge wa sasa wameficha pesa huko Uswisi ndio ni hawa wahindi anajidai ni Watanzania wameficha pesa Uswisi?
Au tuseme Mwanasisa huyu ni mnafiki na muhongo na hafai kusikilizwa? Licha ya kutoa majina hayo pia ukiyatazama utabaini watu wote wenye asili ya bara ya Asia wamefungua Akaunt zao huko nchini Uswis tangu miaka ya Ukoloni yaani wengine mwaka 1935,wengine ni 1956,hivi tusema mwanasiasa huyo alikuwa anamaanisha ni vigogo wa Serikali kipindi cha Ukoloni.
Mbaya Jengine anasema alishindwa kuwataja majina Vigogo wake wa Uswisi akisema atabanwa na sheria,hivi ni sheria hipi anayoisema,kama kweli ulikuwa unahushahidi wa moja kwa moja ulikuwa unaogopa nini kuwataja au vigogo wako.
Dakta Slaa mwaka  2008 alivowataja kwa majina mafisadi papa mbona hatukusikia hata mmoja aliyekwenda mahakamani kumshtaki au kushuhudia akifungwa,yote haya naweza kusema alikuwa na ushahidi wa kile anachokisema lakini wewe Zitto kabwe ulikuwa huna ushahidi.
Yote haya ya kutapatapa inatokana na kuhukumiwa na dhambi ya Usaliti pindu ulipokuwa ndani ya chama cha Demokrasia Chadema ukiwa Naibu Katibu mkuu bara,mara kwa mara umekuwa ukiambiwa ni Mamluki unayetumia na Idara za Usalama za CCM kuja kuharibu chadema .
Sio usaliti hata pindi ulipokuwa Bungeni wakati ulivyokuwa mwenyekiti wa Kamati ya PAC iliyokuwa ikilifuatilia sakata la Wizi wa Mabilioni ya Escrow iliyokuwa Benk Kuu,ulionyesha udhahifu mkubwa.
Udhahifu hule ulitokana aidha ulikuwa wamakusudi au ulifanya vile kwa ajenda Binafsi,maana Kamati yako ilivyozipitia Taarifa za Mkaguzi mkuu wa Serikali iliyokuwa inachunguza sakata hilo pamoja na taarifa ya TAKUKURU ,zote kwa pamoja.
Ila wakati alipokuwa nahiwasilisha Bungeni uliweka wazi kila kitu,lakini aliwataja watu kwa majina waliopewa pesa kupitia benki ya Mkombozi ambao walipewa na Mbia wa Kampuni ya IPTL James Rugimalira peke yao huku kamati hiyo ikawafumbia macho waliopewa pesa zilizofichwa kwenye Akaount Stanbikc Benk.
Tena Benki ya Stanbik tunaambiwa kuwa ndipo vigogo wa Ikulu,Mawaziri hadi wanasiasa wakubwa tu walinufaika na pesa za Escrow lakini la ajabu mwanasiasa huyo na kamati yake aliyokuwa anaiongoza alishindwa kuwataja.

Zaidi aliishia kuwataja watu wasiohusika hata kwa karibu na pengine hata walikuwa hawajui ufisadi huo,tena ni watu ambao walikuwa hawapo kabisa,huko kote kuanzidi kudhilisha mwanasiasa huyo ni kigeugeu na hana nia ya kweli ya kufanya mapinduzi.