MSANII DIAMOND ALIKOROGA TENA,AMCHOKOZA ASKOFU GWAJIMA,SOMA HAPO KUJUA
Mwanamuziki Diamond Platnumz amemuomba msamaha Askofu Gwajima kufuatia kile kilichodaiwa na askofu huyo kuwa ameimbwa kwenye wimbo wa mtu anayepotosha haki ili kutetea vyeti feki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema leo mchana Askofu Gwajima aliandika, “Aliyeniweka kwenye wimbo wa lengo la kupotosha haki ili kusapoti vyeti feki, jiandae, Almasi itageuka maji kesho!”
Kauli hii ya Askofu Gwajima imekuja ikiwa ni saa chache tu tangu mwanamuziki Diamond Platnumz alipotoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Acha Nikae Kimya ambapo ndani ya waliotajwa ni pamoja na Askofu Gwajima. Katika wimbo huo, Diamond alisema kuwa, ugomvi kati ya Makonda na Gwajima unachcochewa na dada mmoja kwenye mitandao.
Baada ya Gwajima kutoka maneno hayo, Diamond amejitokeza na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akifafanua kile alichokiimba kuhusu Gwajima kuwa hakina lengo baya, huku akimtaka Askofu Gwajima kutomgeuza maji kesho kanisani kwake, kwani yeye akimpania mtu huwa hatoki
“Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…” aliandika Diamond na kuongeza;
“Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭 Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁"