Zinazobamba

MAISHA YA WABUNGE YAWA HATARINI,WABUNGE WENGINE WATISHIWA KIFO,SOMAHAPO KUJUA

Idadi  ya wabunge  waliopewa   vitisho   na   watu  wasiojulikana   imezidi   kuwa  hadharani   baada  ya   majina   ya   wabunge   wengine  wanne wapya   kutajwa bungeni   kuwa ni  miongoni  mwa wabunge  ambao  maisha  yao  yapo hatarini  na  hivyo  wanaliomba bunge  kushughulikia   usalama  wao  kwani  hawajui  kwa sasa   watafanyaje  ili kujinusuru  kutoka  katika   hatari  hiyo.

Wakiomba  miongozo   ya    kiti  Mhe.  Mwita  Waitara  mbunge  wa  Ukonga   alitaja  majina ya  wabunge wanne   ambao   alitumiwa   majina   kupitia  ujumbe  wa   mfupi  wa  simu kuwa  wanasakwa  huku Mhe.  Dkt. Godwin  Molley  mbunge  wa  Siha  naye  aliomba muongozo  wa  kiti  kutaka  bunge  liahirishwe  ili wajadili hali hiyo   hata  hivyo  kiti kilikataa   miongozo  hiyo.

Mhe. Said   Kubebea  ni  mbunge  kutoka   Ubungo  ambaye  anasema  kilio  cha  wabunge  kuhusu kuhakishiwa   usalama  wao  ni  jambo  ambalo  mtu  yoyote   hapaswi   kukipuuza kauli  ambayo  inaongezewa  nguvu  na  Mhe. Mwigulu  Nchemba  waziri  wa  mambo   ya ndani  ya  nchi   anasisitiza   usalama   upo  huku waziri wa habari  utamaduni  sana  na michezo  Mhe.  Dkt. Harrison  Mwakyembe  akimjibu Mhe.  Juma  Mkamia kuhusu yeye kushiriki mkutano wa mwanamuziki  Roma Mkatoliki.

Katika   hatua   nyingine  wabunge   wamepata   nafasi  ya  kuchangia  hotuba  ya waziri mkuu  ikiwa  ni katika  hatua  za  kuhitimisha   ambapo   wabunge  wengi wamesema    kama  bajeti   itatekelezwa   kama ilivyopangwa  itakuwa  msaada  mkubwa.