TECNO YAJA NA SIMU BOMBA KABISA,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT.
KATIKA kuhakikisha wanawasaidia watanzania kupata
simu zenye kuwarahisishia mawasiliano katika kipindi hiki nchini inapokwenda
kwenye uchumi wa Viwanda.
Kampuni ya simu inayofanya vizuri nchini ya TECNO
imezindua simu mpya ya Tecno L9 plus ,ambapo wataaramu wanaitaja simu hiyo
kufanya vizuri kwenye soko kutokana na kuja na ufumbuzi wa Tatizo la Chaji.
Akizingumzia simu hiyo Meneja Mauzo rejareja wa
Kampuni ya Tecno,Moses Mtweve amesema lengo la Kampuni hiyo kuzindua simu hiyo
ni kwa ajili ya kuwasaidia watanzania .
“Tecno L9 Puls itakuwa msaada mkubwa kwa watanzania
na wateja wetu kwa ujumla ukizingatia kua umeme katika nchi yetu haujatengemaa
kabisa kwa baaadhi ya mikoa kwahiyo watu wengi wanapata shida ya chaji,kwahiyo
simu hii itawaondolea kadhia hiyo,”amesema Mtweve.
Mtweve ameongeza kuwa simu hiyo itaweza kukaa na
chaji kwa saa 72 huku mtumiajia
akifurahia huduma mbali mbali za mawasiliano.
“Simu ya Tecno kupitia L9 plus inawakikishia wateja
kua watakaa saa 72 bila kuwaza lolote kuhusu chaji huku akiwa anafurahia
huduma,ambapo hata chaji ikiisha ikichajiw akwa dakika tano mtumiajia ataweza
kutumia kwa kupiga picha zaidi ya elfu moja
kwa chaji hiyo ya Dakika tano”ameongeza kusema Mtweve.
Mtweve pia, ametaja faidi nyingine kwa mtumiaji wa
simu hiyo ni kufaudi picha kutokana na simu iyo kuwa na kamera ya nyuma na
mbele pamoja kuwa tecnolojia ya usalama wa vidole.
Hata hivyo,Mtweve amewataka watanzania kujitokeza
kwenye mawakala wa Tecno nchini kujipatia simu hiyo kwa bei nafuu.