Zinazobamba

MAMA MJANE AMVAMIA RAIS MAGUFULI JUKWAANI,SOMA HAPO KUJUA



 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa kimahakama, Bi Sobha Mohamedi ameibua taflani  na kugeuka shujaa mara baada ya kufanikiwa kuelezea tuhuma zake kwa namna alivyodhurumiwa haki zake katika mahakama ya mwanzo mkoani Tanga.

Sobha ambaye alifanikiwa kupenya katikati ya watu na kusogea mbele akiwa na bango ambalo lilikuwa likieleza jinsi alivyodhulumiwa kisha kuzuiwa na walinzi wa Rais lakini Rais Dk John Pombe Magufuli akaamuru asogee mbele asikilizwe.


Mama huyo mara baada ya kufika mbele ya Rais aliweza kueleza kila kitu na mwenendo wa jinsi kesi yake ilivyokwenda na hatimaye kupewa hukumu ambayo ilikuwa ya pande mbili ambayo haitoi haki ya moja kwa moja ya  kuendelea kuwa mmiliki wa mirathi aliyofungua.

Mara baada ya kujieleza hivyo Rais Magufuli aliagiza mamlaka zote kuhakikisha kuwa mahakama na mamlaka zinazo husika kushughulikia kesi hiyo kuhakikisha kuwa haki inatendeka .


Dk Magufuli ameagiza jeshi la Polisi kumpatia mama huyo ulinzi ili aweze kuishi kwa amani bila kubugudhiwa na mtu yeyote,huku akiendelea kutunza ushahidi wa kesi hiyo.