TAASISI YA KAREMJEE JIVANJEE FOUNDATION YATOA ZAWADI YA UFADHILI WA MASOMO KWA WANAFUNZI WA TANZANIA,SOMA HAPO KUJUA
Nadhra Mresa akikabidhiwa zawadi yake kutoka kwa Yusuph Karimjee wakati wa Hafla Fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao.
Taasisi
ya Karimjee Jivanjee Foundation imewapatia zawadi Diana sosoka na Nadhra Mresa
ambao ni wanafunzi wa shule ya secondary ya wasichana Mtwara kwa kuibuka
washindi wa kwanza kwenye mashindano ya wanasayansi chipukizi Young Scientist
Tanzania (YST) kwa mwaka 2016.
Akizungumza
na wahabari wakati wa Hafla ya kuwaaga washindi hao wanaoelekea katika Jiji la
Dublin nchini Ireland kwa niaba ya mwenyekiti wa KJF Yusuph Karimjee amesema
kuwa wawili hao watapata ufadhili wa masomo wa elimu ya juu pindi
watakapohitimu masomo yao ya kidato cha sita.
Diana
sosoka Mshindi wa shindano la wanasayansi chipukizi akikabishiwa zawadi
yake kutoka kwa Yusuph Karimjee leo Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa taasisi hiyo ya KJF amesema kuwa wao wanafuraha kubwa kuwa moja kati ya
wafanikishaji wa wanafunzi hao kutimiza ndoto zao za kimasomo hasa kiwango chao
cha masomo ya sayansi jambo ambalo linapiganiwa na dunia nzima kuwa na
wanasayansi wengi.
Wanafunzi
hao kutoka Mtwara secondary waliibuka kidedea baada ya kueleza wazo lao la
kutaka kuwasaidia kina mama wa mkoa wa mtwara kuondokana na umasikini waliokuwa
nao kwa kuwafundisha ufugaji wa kisasa wa kutotolesha kuku ambao wanaweza
kuutumia katika kujikwamua na umaskini ulio mkubwa
.
.
Wasichana hao
walishiriki mashindano ya wanafunzi mbalimbali wanasayansi yaliyoandaliwa na
Taasisi ya young scientist Tanzania TYS Ambapo yalishirikisha wanafunzi kutoka
shule mbalimbali nchini Tanzania wakionyesha ubunifu mbalimbali wa kisayansi
ambao wamebuni.
Wakizungumza
na wanahabari wasichana hao wamesema kuwa masomo ya sayansi yamekuwa
yakionekana kama ni magumu sana hasa kwa watoto wa kike jambo ambalo wamesema
sio kweli bali kinachihitajika ni juhudi za kweli na nia ndiyo itakayomsaidia
msichana mwanafunzi kufikia malengo yake.