RAIS WA MAREKANI APINGWA MAHAKAMANI,NI TRUMP,SOMA HAPO KUJUA

Mahakama moja ya New York Marekani imeridhia ombi la
wanaharakati waliokwenda Mahakamani kupinga amri ya Rais Donald Trump wa nchi
hiyo, kupiga marufuku Wakimbizi wa Syria na raia wengine wa nchi sita za
kiislamu kama Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen wasiingie Marekani.
Mahakama hiyo imeamuru wote waliozuiliwa kupitia
amri hizo waachiwe ikiwa ni agizo la lililotolewa saa kadhaa baada ya kuwepo
Ripoti kutoka uwanja wa ndege wa John F Kennedy New York kwamba watu kadhaa
wamezuiwa kuingia Marekani wakiwemo wale ambao walikuwa wamepewa ruhusa kwenda
kuishi Marekani kupitia mpango maarufu wa Green Card.
Tayari pia Raia wawili wa Iraq wameishitaki
Mahakamani serikali ya Marekani baada ya kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa
John F. Kennedy New York na kuzuiwa kuingia Marekani ambapo inaripotiwa wakati
huo kuna raia wengine 10 walikua wamezuiwa kuingia Marekani muda mfupi tu baada
ya ndege kutua