Al-Shabab Washambulia kambi ya Wanajeshi wa KENYA Nchini Somali na Kuwaua 57
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limesema
wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya
kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.
Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye
shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa
nchi hiyo na Kenya.
"Mujahideen (wapiganaji) wawili
walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi
hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya
makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi,"
mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la
habari la Reuters.

Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi
zaidi ya 57 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji
wa majeshi ya Kenya amekanusha.
Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters: "Ni
uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa."
Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya
serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na jamii ya kimataifa.
Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka
Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali
hiyo yenye makao yake Mogadishu.
Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab
walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.
Al-Shabab walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100.
Jeshi la Kenya halijatangaza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.
Chanzo: BBC
Chanzo: BBC
Post Comment