WATU 14 AKIWEMO MCHINA MMOJA WAHOFIWA KUFA BAADA YA KUFUKIWA KWENYE MGODI WA MADINI,SOMA HAPO KUJUA

Watu 14 akiwemo Mchina, wanahofiwa kufa baada ya
kufukiwa katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata
ya Nyarugusu mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga jana alisema
watu hao wamefukiwa chini ya mgodi baada ya mlango wa kuingilia kwenye shimo la
mgodi kumeguka udongo na kujiziba.
“Usiku wa kuamkia leo (jana) saa tisa
kwenye mgodi huo unaoendeshwa na Wachina, mlango wa kuingilia mgodini mmoja
ulimeguka na kujifunga watu 14 wakiwa ndani,” alisema
Kyunga.
Kyunga alisema kwa mujibu wa kitabu cha orodha ya
watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina.
Aidha, alisema mbali na watu hao 13, pia kuna
Mtanzania mmoja ambaye aliingia bila kujiandikisha na hiyo ni kwa mujibu wa
watu walioshuhudia tukio hilo hivyo kufanya idadi ya watu waliofukiwa kuwa
14.
Kyunga alisema tangu jana asubuhi jitihada
mbalimbali za kuondoa udongo kuwaokoa watu hao zinaendelea wakitumia mitambo na
wataalamu.
“Kwa kusaidiana na Kampuni ya Geita Gold
Mine (GGM) na wataalamu wengine, jitihada zinaendelea ili kuhakikisha
tunawaokoa watu hao,” alisema Kyunga.
Alisema wakati huo huo wamefanikiwa kutoboa eneo
jingine na kupitisha mabomba ya hewa ya oksijeni ili kuwafanya watu hao
wasikose hewa
Post Comment