WAZIRI NAPE ALIA NA MAADILI KWA WATUMISHI,SOMA KUJUA
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
na watumishi wa Wizara yake wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi
la Wizara katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel akizungumza katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara
hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam Desemba 08, 2016.
Mwenyekiti
wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi
Magreth Mtaka akitoa hoja za wafanyakazi katika kikao cha Baraza la
wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel akipokea hotuba ya wafanyakazi kutoka kwa Mwenyekiti wa TUGHE
Tawi la Wizara hiyo Bibi Magreth Mtaka katika kikao cha Baraza la
wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar
es Salaam Desemba 08, 2016.
Baadhi ya wawakilishi wa watumishi wa Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Taasisi zake wakifuatilia kikao
cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Wizara yake mara
baada ya kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Na Raymond Mushumbusi -WHUSM
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka
watendaji na watumishi wa Wizara yake kuzingatia maadili na uwajibikaji
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Ameyasema
hayo wakati akifungua Baraza la wafanyakazi la Wizara yake na
kusisitiza kwa watendaji kuwasimamia watumishi walio chini yao
kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao
katika kutoa huduma kwa wananchi.
Ameongeza
kuwa kuwepo kwa ushirikiano kati ya uongozi na watumishi utasaidia
kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo ya Wizara, Taasisi zake na
watumishi katika kuleta maendeleo ya Wizara katika kutimiza wajibu wao.
“Nawataka
watumishi wazingatie maadili katika kutekeleza wajibu wao na naamini
kwa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano tutarudisha maadili ya Utumishi
wa Umma na bado taratibu zinaendelea kusimamiwa ipasavyo”asisitiza Mhe
Nnauye.
Mhe.
Nnauye amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt John Pombe Magufuli ana mpango wa dhati wa kurujesha maadili katika
Utumishi wa Umma na kuhakikisha heshima yake inarudi.
Alieleza kuwa endapo kuna mtumishi yoyote atakayeshindwa kusimamia suala zima la maadili anapoteza utumishi wake.
“
Wananchi ndiyo tunaowatumikia na ndiyo wanaotufanya tuwepo hapa tulipo
wanahitaji huduma bora. Kama hatutazingatia suala la maadili ni hakika
hatutaweza kuwatumikia vema” alieleza.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara hiyo , Prof Elisante Ole Gabriel
ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa kuhakikisha watumishi wanazingatia
maadili na suala hili linafanyika kwa vitendo zaidi na sio maneno ili
kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli za kurudisha maadili katika
Utumishi wa Umma.
“Mhe.
Waziri nakuahidi mimi pamoja na watendaji wenzangu tutalisimamia suala
hili na kulitekeleza kwa vitendo ili turudishe heshima ya utumishi wa
Umma kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kurudisha uaminifu kwa
wananchi”alisema Prof Gabriel.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Bibi Magreth Mtaka amesema kuwa ni jambo muhimu kwa
watumishi kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao katiKa
eneo la kazi.
“Niwashauri
watumishi wenzangu tuzingatie maadili ya Utumishi wa Umma ili turudishe
heshima ya utumishi wa umma na tutoe huduma iliyo bora kwa wananchi”
alisema Bibi Magreth.