RAIS MAGUFULI AWASAMEHE WAFUNGWA KIBAO,SOMA HAPO KUJUA
Katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania
Bara tarehe 9 Disemba, 2016 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-
(i)
Wafungwa wote wamepunguziwa moja ya sita (1/6) ya vifungo
vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha Sheria
ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2
(i-xx).
(ii)Wafungwa
wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na SARATANI (CANCER)
ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa ambao wamethibitishwa na Jopo la
Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.
(iii)Wafungwa wazee wenye umri wa miaka
sabini (70) au zaidi ambao umri huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya
Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.
(iv)Wafungwa wa kike walioingia na mimba
gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.
(v)Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na
akili (Physical disability and mental disability) ambao ulemavu huo
umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa
Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.
2.Aidha, Msamaha huu wa Mheshimiwa Rais hautawahusu
wafungwa wafuatao:-
(i)Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya
kunyongwa.
(ii)Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya
kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo
gerezani.
(iii)Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha
maisha gerezani.
(iv)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa
makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama
vile cocaine, heroin, bhangi n.k.
(v)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa
makosa ya kujihusisha na uombaji, upokeaji au utoaji rushwa.
(vi)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa
makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda
makosa hayo (robbery with violence, armed robbery and attempt robbery).
(vii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa
makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali (firearms,
ammunitions and explosives).
(viii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa
makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti, au kujaribu kutenda
makosa hayo.
(ix)Wafungwa waliopatikana na hatia na
kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na
Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na
nane (18) na kuendelea.
(x)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa
ya wizi wa magari na pikipiki au kujaribu kutenda makosa hayo.
(xi)Wafungwa wanaotumikia kifungo chini
ya Sheria ya Bodi ya Parole (Act. No. 25/1994) na Sheria ya Huduma kwa Jamii
(Act. No. 6/2002).
(xii)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa
kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao.
(xiii)Wafungwa waliowahi kupunguziwa
kifungo na Msamaha wa Mheshimiwa Rais na bado wangali wanaendelea kutumikia
sehemu ya kifungo kilichobaki.
(xiv)Wafungwa waliopatikana na hatia na
kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo.
(xv)Wafungwa waliopatikana na hatia na
kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, kupoka na kufanya biashara ya
binadamu (Human Trafficking).
(xvi)Wafungwa waliopatikana na hatia na
kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.
(xvii)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa
makosa ya kujihusisha na usafirishaji wa nyara za Serikali na ujangili
(Poachers).
(xviii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa
makosa ya wizi/ubadhirifu wa fedha za
Serikali.
(xix)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa
makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali.
(xx)Wafungwa walioingia gerezani baada ya tarehe
9/10/2016.
3.Wafungwa wapatao 5,678 watafaidika na msamaha huu baada ya kupunguziwa 1/6 ya vifungo vyao
ambapo 1,340 wataachiliwa huru na wafungwa 4,338 watanufaika na kubaki gerezani
wakitumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.
Ni mategemeo ya
Serikali kwamba watakaoachiliwa huru watarejea tena katika jamii kushirikiana
na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili
wasirejee tena gerezani.
Imesainiwa na;
Meja Jenerali Projest
Rwegasira
KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO
YA NDANI YA NCHI
9/12/2016