MFUMKO WA BEI JUU,OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATAJA CHANZO,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
|
mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii
Epharaim Kwesigabo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) leo Jijini dar es Salaam,kuhusu hali ya
mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba mwaka huu, kulia kwake ni Mtakwimu Bw.
Muhidini Mtindo.
|
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba 2016
umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5 iliyokuwapo
mwezi Octoba, 2016 kutokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa na
huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa bidhaa za vyakula zikiwemo ngano,mbogamboga,
mtama, na vinywaji baridi zimechangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei
nchini.
“Bidhaa nyingine zilizochangia kuongezeka kwa
mfumuko wa bei nchini ni Nishati , mafuta na viatu huku akibainisha kuwa
kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa
na kaya nchini zimeongeka na kufikia 104.32 kwa mwezi Novemba 2016
ikilinganishwa na 99.54 za mwezi Novemba mwaka jana” Amesema Kwesigabo.
Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo
cha mwezi ameeleza kuwa umeongezeka kwa asilimia 1.1 kwa mwezi Novemba
ikilinganishwa na asilimia 0.1 ya mwezi Octoba kutokana na kuongezeka kwa
Fahirisi ya baadhi ya bidhaa zikiwemo unga wa ngano, unga wa mihogo, unga wa
mahindi, mtama, dagaa, mchele.
Aidha, alisema kuwa thamani ya shilingi ya Tanzania
hupima badiliko katika kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo
shilingi ya Tanzania ingeweza kununua katika kipindi tofauti, ikiwa fahirisi za
bei za Taifa zinaongezeka uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa
na huduma hupungua.
Kwa upande wa mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi
ya nchi za Afrika Mashariki Kwesigabo alisema kuwa una mwelekeo
unaofanana ambapo Kenya umeongezeka na kufikia asilimia 6.68 mwezi
Novemba kutoka 6.42 za mwezi Octoba huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei wa
asilimia 4.6 mwezi Novemba kutoka asilimia 4.5 za mwezi Octoba.
