WASIOMTAKA RAIS SHEIN WAANZA KUKAMATWA,AANZA KUTUMIA MAJESHI KUZULU MISIKITINI,SOMA HAPO KUJUA
WASIOPENDA kusikia jina la Dk. Ali Mohamed Shein,
Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa makubaliano ya uongozi wa msikiti wao, sasa
wamekamatwa, anaandika Mwandishi Wetu.
Waliokamatwa
na Serikali ya Dk. Shein wanatajwa kuwa wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF)
ambao ni waumini wa Msikiti wa Kijiji cha Kangagani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa
Kaskazini Pemba.
Ijumaa ya wiki iliyopita kwenye msikiti huo
kuliibuka mgogoro baada ya mtoa mawaidha wakati wa Swala ya Ijumaa kutaja jina
la Dk. Shein kinyume na makubaliano ya waumini wa msikiti huo waliopiga
marufuku kutajwa jina hilo.
Wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi ni Salum Hamda
Simba (37), Jamal Hamdi Khatibu (40), Khatib Jamal Jabu (62) na Ali Dogi (44).
Haji Khamis Haji, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kaskazini Pemba amethibitisha kukamatwa kwa watu hao.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, waumini wa msikiti
huo walikubaliana kutotajwa jina la Dk. Shein kwenye msikiti huo kutokana na
makovu ya kisiasa yaliyotokea kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.
Mzozo ulianza baada ya jina la Dk. Shein kutajwa
ndani ya msikiti huo huku waumini wakionesha kukerwa kwa mtoa mawaida huyo,
taratibu mzozo ukaanza kuibuka.
Hata hivyo, kabla ya vurugu kuwa kuwa, baadhi ya
waumini kutokana na kukerwa na jina la Dk. Shein ndani ya msikiti huo, waliamua
kutoka nje.
Ilipofika usiku wa saa tatu, Jeshi la Polisi
lilivamia msikiti huo uliogomea kutajwa jina la Dk. Shein na kuanza kupiga
mabomu.
Baada ya polisi kuvamia na kupiga mabomu, hali ya
taharuki ilitanda na kusababisha watu wanaoishi jirani na msikiti huo kuanza
kukimbia.
Said Ahmad Muhammad, Ofisa wa Ofisi ya Mufti wa
Taasisi ya Kiislam anayeshughulikia Fatwa (maamuzi) alinukuliwa akisema, kuwa
mgogoro kwenye msikiti huo anaujua.
Na kwamba, pande hizo zilieleza umuhimu wa
kutuingiza masuala ya kisiasa kwenye nyumba za ibada.
Hata hivyo, baada ya pande hizo mbili kuelezwa
umuhimu wa kutenganisha siasa na ibada, walikubaliana kuwa Dk. Shein hatotajwa
tena kwenye msikiti huo na kuwa, alishangaa jina hilo kutajwa kinyume na
makubaliano.
Chanzo ni Mwanahalisi oline