Waajiri waagizwa kuwasilisha makato ya Fidia kwa Wakati
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mh. Jenista
Mhagama akiongea na wadau mbalimbali (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi
wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
(jana). (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mh. Jenista
Mhagama akizindua Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Kushoto ni Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Watu Wenye Ulemavu Mh. Dkt. Abdallah
Possi uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana). (Picha na
Benjamin Sawe-Maelezo).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mh. Jenista
Mhagama akisoma ujumbe mara baada ya kuzindua Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo (jana). (Picha na Benjamin
Sawe-Maelezo).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mh. Jenista
Mhagama akikabidhi Tuzo ya Ushiriki kwa mmoja wa wadau waliohudhuria
hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi uliofanyika jijin
Dar es Salaam leo (jana). (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi Masha Mshomba akiongea na wadau mbalimbali kabla
ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es
Salaam leo (jana). (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi Emanuel Humba akiongea na wadau mbalimbali kabla
ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es
Salaam leo (jana). (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Kazi Mh. Jenista
Mhagama wakati wa Mfuko huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana).
(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mh. Jenista
Mhagama (wanne kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na
Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali baada ya
uzinduzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es
Salaam leo (jana). (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Kazi Mh. Jenista
Mhagama wakati wa Mfuko huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
(jana). (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mh. Antony Mavunde akiongea na wadau
mbalimbali (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana). (Picha na
Benjamin Sawe-Maelezo).
…………………………………………………………………………………
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO-Dar es Salaam
SERIKALI imewaagiza Waajiri wote
nchini kuwasilisha kwa wakati michango ya mafao ya fidia kwa wafanyakazi
ili kuwawezesha watumishi wao kupata huduma za matibabu pindi
watakapoumia au kuugua wakiwa katika maeneo yao ya kazi.
Agizo hilo limetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Ajira, Kazi na Ulemavu) Jenister Mhagama wakati alipokuwa akizindua
huduma za utoaji wa mafao ya fidia na ubia baina ya mfuko wa fidia kwa
wafanyakazi (WCF) na watoa huduma za afya nchini.
Mhagama alisema suala la
uchangiaji wa mafao hayo sio la hiari ila lipo kisheria na hivyo ni
wajibu wa waajiri wote nchini kuhakikisha kuwa wafanyakazi wao
wanaingizwa katika mfumo huo ili kuwawezesha wafanyakazi kuwa na uhakika
wa kulipwa fidia pindi wanapokuwa kazini.
“Katika mwaka wa fedha 2016/17
Serikali imelipa michango yote ya wafanyakazi wake, na huu ni mfano
unaopaswa kuigwa na waajiri wengine nchini, na natoa rai kwa Chama cha
Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA)
linasimamia suala hili” alisema Mhagama.
Aidha Mhagama alisema lengo la
kuanzishwa kwa mfuko huo wa wafanyakazi nchini ni kusaidia kutatua kilio
cha muda mrefu cha wafanyakazi wa sekta za umma na binafsi, ambao
wamekuwa wakilalamikia huduma hafifu zinazotolewa pindi wapatapo majanga
mbalimbali wakiwa kazini ikiwemo ajali na vifo.
Waziri Mhagama alitaka Bodi ya
mfuko huo kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria zilizopo ili
kuhakikisha kuwa waajiri wote hususani wa sekta binafsi wanawasilisha
michango kwa wakati.
Akifafanua zaidi Waziri Mhagama
aliuataka mfuko huo kujitangaza zaidi kwa sekta zisizo rasmi ili
kuwawezesha wananchi wengi zaidi hususani wa kipato cha chini kujiunga
na mfuko huo na kuwasaidia kufaidi huduma zinazotolewa.
“Natoa rai kwa mifuko yote ya
hifadhi ya jamii nchini ikiwemo wa WCF mjitangaze katika sekta zisizo
rasmi ikiwemo waendesha bodaboda, akina mama lishe, kwa kuwa idadi yao
ni kubwa na hiyo itawezesha kupata wanachama wengi zaidi” alisema
Mhagama.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko huo, Masha Musomba alisema hadi kufikia sasa mfuko huo umeweza
kutoa usajili wa waajiri 5945 pamoja na kuendesha mafunzo mbalimbali ya
kuwajengea uwezo watumishi wa mfuko huo ikiwemo madaktari.
Aidha Musomba anasema pia mfuko
huo umeingia ubia na taasisi 7 za utoaji huduma za afya nchini, ambazo
ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Taasisi ya Mifupa Muhimbili
(MOI), na Taasisi ya Kansa ya Ocean Road.
Musomba anazitaja taasisi
nyingine kuwa ni Strategis, AAR, mfuko wa Jubilee, na Hospitali ya Taifa
Muhimbili, ambapo taasisi hizo zinazoendelea kushughulikia kesi 189
zilizolipotiwa katika mfuko huo.
Naye Mtendaji Mkuu wa Chama cha
Waajiri Nchini (ATE), Aggrey Mwinuka alisema mfumo huo wa fidia umekuja
katika wakati muafaka kwa kuwa sheria zilikuwepo katika vitabu na
hazikuwa na utekelezaji uliokusudiwa.
Mwinuka alisema ili kuhakikisha
kuwa malengo ya mfuko huo yanatekezeka ni wajibu wa Serikali kuhakikisha
kuwa inafanya majadiliano ya mara kwa mara na waajiri ili kuangalia
viwango vya makato ya michango ya wafanyakazi wa sekta ya umma na
binafsi.
Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo,
Emmanuel Homba alisema uwekaji wa mfumo wa mafao ya fidia utawezesha
wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi kuchangia kikamilifu katika
Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya ujenzi wa uchumi wa viwanda
nchini.