TUKIO ALILOFANYA RAIS MAGUFULI KIJIJINI KWAKE CHATO,SOMA HAPO KUJUA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
29 Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani
Geita kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
ambaye ni mzee maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye
ni jirani yake.
Rais
Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa
kuondokewa na mpendwa wao pia amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea
kuishi kwa kushikamana na kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa
marehemu na kuwataka kuepukana na mifarakano.''Unapotokea msiba kama huu katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu kwenu wewe Mama mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa kutokana na kifo cha mume wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee kuishi kwa kupendana kama enzi za uhai wa mzee''
Aidha Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa mzee maarufu kijijini hapa na miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare zake za shule wakati akisoma.
Kwa upande wake Mdogo wa marehemu ambaye ni msemaji wa familia Bwana Deodatus Manyama ambaye ni msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kuwapa pole katika msiba huo, na kwamba kitendo hicho kinaonyesha kuwa Rais magufuli si mtu asiejikweza wala asiye na majivuno.
Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha wajane wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
29 Desemba, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee
Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa
marehemu Chato mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee
Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu
Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee
Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato
mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la
maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe
Manyama (82) Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu MzeeAdmirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.