SUALA LA USHOGA LAIUMIZA KICHWA SERIKALI YA JPM,MWIGULU AJIAPIZA ,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
ametaka apewe taarifa kuhusu taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO)
wanaohamasisha au kutangaza ndoa za jinsia moja nchini ili azifutie usajili
mara moja.
Aidha ametaka kutajwa kwa watu wanaojihusisha na
vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa kujihusisha na vitendo
hivyo ambavyo vinapigwa vita dunia nzima.
Nchemba aliyasema hayo jana mjini Kibaha alipokuwa
akizungumza na taasisi za Kijeshi za mkoa huo zikiwemo Uhamiaji, Polisi,
Magereza na Zimamoto juu ya kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Alisema kuwa taasisi hizo hazifai kwani zinafanya
kazi ya laana ambayo ni kinyume cha maadili ya Kitanzania na hazistahili
kuendelea kufanya kazi kwa upotoshaji huo.
“Leteni majina ya taasisi hizo ili tuzifute kwani
hazistahili kuendelea kufanya jambo hilo ambalo ni laana na halipaswi kufumbiwa
macho ndani ya jamii,” alisema Nchemba.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi
alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja
na upungufu wa vitendea kazi, ikiwa ni pamoja na magari.
Mushongi alisema kuwa licha ya kukabiliwa na
changamoto hizo wamekuwa wakikabiliana na uhalifu kwenye mkoa huo ambao umekuwa
kimbilio la wahalifu kutoka mikoa jirani ya Dar es Salaam.