PAMBANO LA MBUNGE LEMA NA MAWAKILI WA SERIKALI LAFIKIA PATAMU,AZIDI IBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, imelikubali ombi
la Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, la kuongezewa muda wa
kuwasilisha Notisi ya nia ya kukata rufaa ya dhamana yake.
Akitoa uamuzi wake kuanzia saa 12:26 hadi saa saba
mchana, Jaji Dk. Modesta Opiyo wa Mahakama hiyo, alisema Mahakama hiyo
imeruhusu maombi ya kuwasilisha Notisi ya kuomba kuongezewa muda wa kuwasilisha
notisi ya nia ya kukata rufaa ya dhamana yake.
Jaji Opiyo amesema hoja za Upande wa serikali
zilizowasilishwa na Wakili Hashim Ngole za kudai waleta maombi hayo walikuwa
wazembe na walichelewa siku nne kuwasilisha Notisi baada ya rufaa yao
kuondolewa na Jaji Fatuma Masengi Desemba 2 hazina mashiko.
Alisema kuondoa kesi mahakamani haimaanishi
kuwanyima fursa ya kupigania nia ya kukata rufaaa, bali milango inakuwa wazi
haijafungwa.
Aidha amesema siku nne zinazolalamikiwa kuwa
walichelewa kutoa maombi hayo, mahakama inaona hoja hizo hazina mashiko sababu
siku mbili kati ya hizo zilikuwa siku za mapumziko Jumamosi na Jumapili, hivyo
walitumia siku mbili kuandaa nyaraka na kuleta maombi hayo.
Pia alisema katika maombi hayo wametoa pia sababu za
nia ya kutaka kukata rufaa na sababu hizo ziko wazi.
“Katika hili hakuna uvunjifu wowote wa
sheria uliofanywa na kutokana na hilo Mahakama hii inatumia busara zake
kuruhusu maombi haya ya kutoa Notisi ya kuomba kuongezewa muda wa kukata rufaa
juu ya dhamana yake Mbunge huyu,” alisema Jaji Opiyo.
Amesema Mahakama inatoa siku kumi pekee kuanzia
uamuzi huo utolewa mleta maombi (Lema) kuwasilisha Notisi yake ya kuomba
kuongezewa muda wa kukata rufaa hadi tarehe 30 shauri hili likakaposikilizwa
tena.
Baada ya kutolewa kwa maamuzi hayo, tayari Wakili
Sheck Mfinanga ameshakata Notisi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kupokelewa.
Mfinganga amesema wanasubiri mahakama ili wapangiwe
Jaji waendelee na kesi hiyo ya hatma ya dhamana ya Lema.