SHEIKH PONDA AWASHANGAZA WENGI,ASAFIRI TOKA DAR MPAKA ARUSHA KUMJULIA HALI MBUNGE LEMA,SOMA HAPO KUJUA
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh
Ponda Issa Ponda amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema
katika Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha la Kisongo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Vijana
la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Noel Olevaroya, Sheikh Ponda
alizungumza na Lema kwa muda usiopungua saa moja.
“Sheikh Ponda amekutana na Mbunge wetu
Lema na amekuja mahususi kumjulia hali na amemuambia hampi pole bali
anampongeza kwa kukaa mahabusu muda wote licha ya kuamini anastahili kupata
dhamana,” alisema Olevaroya.
Alisema katika mazungumzo yake alimtaka Lema kuwa
sauti ya wanyonge kwa kuzungumza hata kama itamfanya awe sehemu alipo hivi
sasa, kwani kuna mambo mengi yanayohitaji kusemwa na hakuna wa kuyasema.
Pia, alimsihi kutokuona kama ametengwa bali hiyo
ndiyo njia ya wapigania haki na demokrasia wanayopitia, akijitolea mfano yeye
binafsi.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani
Golugwa alipotafutwa kwa njia ya simu hakupokea na alipotumiwa ujumbe mfupi
hakuweza kujibu iwapo chama chake kilikuwa na taarifa ya ugeni wa Sheikh Ponda
au ilikuwa ni safari binafsi.
Atuma salamu za harusi
Katika hatua nyingine Lema aliandika barua yenye kumbukumbu namba 76/AR/I/I/36 akimtakia heri ya ndoa, Wakili wa chama hicho, John Malya.
Katika hatua nyingine Lema aliandika barua yenye kumbukumbu namba 76/AR/I/I/36 akimtakia heri ya ndoa, Wakili wa chama hicho, John Malya.
Katika barua hiyo iliyowekwa muhuri na Ofisa wa
gereza hilo, Lema alimtumia Malya salamu hizo katika ndoa yake iliyofungwa
juzi, Jumamosi.
“Harusi yenu ni Jumamosi tarehe
10/12/2016 na kwamba nadhani sitaweza kuhudhuria, ningependa sana kuwepo,
nimeshindwa kusimamia na hata keki sili? Niko gerezani Arusha,” ilinukuliwa
sehemu ya barua hiyo.
Barua hiyo iliendelea: “Natamani kuona jinsi
mlivyovaa kwani nilikuwa nimepania sana, lakini najua mtakuwa mmependeza sana
ninawaombea kwani huku jela nina nafasi sana ya kuomba kwa kweli, naomba hadi
Mungu anafurahi.”
Lema ambaye alikamatwa Novemba 2, akiwa Dodoma, hadi
sasa anashikiliwa katika gereza hilo kutokana na kusudio na Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP) la kupinga uamuzi wa hakimu mkazi, Desdery Kamugisha aliyempa
dhamana Lema katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi
dhidi ya Rais John Magufuli.
Katika kesi hiyo, ambayo huvuta umati, Lema anatuhumiwa kati ya Oktoba 23 hadi 26 kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais Magufuli katika maeneo tofauti na mikutano yake ya hadhara.
Lema anadaiwa katika maeneo matatu tofauti alitoa
maeneo ya uchochezi kuwa: “Nchi itaingia katika machafuko kama haitafuata misingi
ya katiba na sheria na pia Rais Magufuli asipobadilika.”
Lema pia akiwa katika Uwanja wa Shule ya Sekondari
Baraa anadaiwa kutoa kauli kuwa: “Kiburi cha Rais akiendeea kujiona yeye ni
Mungu, hatafika 2020, Mungu atakuwa amechukua maisha yake, Rais ni mbabe na
watu anawaonea, wafanyakazi wa Serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana
amani.”
Alisema Lema akiwa katika Uwanja wa Kambi ya Fisi
Kata ya Ngarenaro alitoa kauli kuwa: “Rais akiendelea tabia ya kud- halilisha
demokrasia na uongozi wa upinzani ipo siku taifa litaingia kwenye umwagaji wa
damu, Rais yoyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, katiba, atakuwa
ameliingiza taifa katika majanga na umwagaji wa damu, watu wamejaa vifua
wakiamua kulipuka polisi hawana uwezo na jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu
utakapotea.”