LOWASSA AENDELEZA UPENDO WAKE KWA WAISLAM,SOMA HAPO KUJUA
Nachukua nafasi hii kuwatakia kheri na baraka
waislam wote nchini katika kuadhimisha siku hii ya kuzaliwa kwa kiongozi wao
Mtume Muhammad SAW.
Waislam kama walivyo watanzania wa dini nyingine
wamekuwa nguzo muhimu katika kujenga amani, upendo na utulivu nchini kwetu, na
hii yote ni kutokana na mafundisho ya kiongozi wao huyo.
Ni rai yangu kwa watanzania wote wakiwemo watawala
kuwa tunapo sherehekea siku hii tutimize kwa vitendo mafundisho ya bwana Mtume
ambaye ni mmoja wa mitume wa mwenyezi mungu kwa kuheshimiana, kuvumiliana na
kupendana.
Edward Lowassa
Waziri mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati
Kuu - Chadema.