SERIKALI YA MAGUFULI YAJITETEA KUHUSU TUHUMA HIZI KWA WATUMISHI WA UMMA,SOMA HAPO KUJUA
Kumekuwa na taarifa inasambazwa katika mitandao ya
kijamii, makundi ya ‘WhatsApp’, ‘Facebook’ na majukwaa mbalimbali ikieleza kuwa
Serikali imepiga marufuku watumishi wa umma kukopa Benki,SACCOS,VICOBA na
Taasisi mbalimbali za kifedha.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Desemba 2016 na
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeeleza kuwa taarifa inayosambazwa, ambayo
imetafsiri mawasiliano ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni ya
kupotosha, hivyo watumishi wote wa umma wanaombwa kuipuuza.
Vilevile watumishi wa umma wametakiwa kuzingatia
kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali HAINA mamlaka ya kuzuia wala
kuruhusu mtumishi yeyote wa Serikali kukopa au kutokopa katika Taasisi yoyote
ya Fedha nchini.
Watumishi wa umma pia wamekumbushwa kuwa mikopo yote
ya watumishi wa umma katika Taasisi za Fedha hutolewa kwa kuzingatia Sheria,
Kanuni na taratibu zilizopo ili mradi mtumishi awe ametimiza vigezo.
Aidha, watumishi wa umma wameaswa kuacha tabia ya
kusambaza taarifa zisizo za kweli na ambazo zina mamlaka husika ya kuzitoa
ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma