SAKATA LA AJIRA ZA SERIKALI LAZIDI KUWA SINEMA,WALIOFANYIWA USAILI NA KUPITA WATAKIWA KUANZA KUOMBA TENA,SOMA HAPO KUJUA
Watu wote waliokuwa wamefanya usaili kwa ajili ya
ajira serikalini kupitia Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma kabla ya
ajira kusimamishwa, watafutwa ndani ya miezi 6 na kulazimika kuomba upya kipindi
ajira hizo zitakapotangazwa tena.
Hilo limebainishwa na sekretarieti hiyo kupitia
majibu kwa wadau mbalimbali kwa mwezi Desemba ambao wamekuwa wakiuliza maswali
na kujibiwa kila mwezi kupitia tovuti yake, na kubainisha kuwa suala hilo
litawahusu wale ambao walifaulu usaili lakini kabla hawajapangiwa vituo vya
kazi au kupewa barua na waajiri wao, ajira zikasimamishwa ili kupisha uhakiki
wa watumishi hewa.
Taarifa hiyo imesema kuwa huo ni utaratibu wa
kawaida wa sekretarieti hiyo, kwamba majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye
kanzi data (Database) kwa muda usiozidi miezi sita, na baada ya hapo majina
hayo hufutwa.
"Kwa mujibu wa Taratibu zetu za
uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya waombaji kazi waliofaulu lakini
hawakupangiwa vituo vya kazi kwa sasa huhifadhiwa kwenye kanzi data kwa muda
usiozidi miezi sita" Imesema taarifa hiyo
Swali lingine kutoka kwa mdau na jibu
lake liko kama ifuatavyo:-
Kwa kuwa ajira zilisitishwa mwezi Juni, na sasa ni
mwezi Desemba, utaratibu huo unamaanisha kuwa wasailiwa wote waliofaulu lakini
hawakupangiwa kazi, watalazimika kusubiri upya matangazo ili waombe upya na
kufanya usaili upya.
Aidha Sekretariet hiyo imebainisha kuwa zoezi ya
uhakiki wa watumishi hewa bado linaendelea, na kwamba wakipewa ruhusa ya
kutangaza ajira wakati wowote watatangaza.