NAIBU WAZIRI JAFFO AWAFUNDA WATUMISHI WA MANISPAA YA ILALA,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Utumishi na Utawala bora ,Seleman Jafo amewataka
watumishi Halimashauri ya Manispaa ya Ilala kutimiza majukumu yao kikamilifu
ili kuchochea maendeleo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa
Anatoglo alipokuwa anazungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo wakiwemo
madiwani, wakuu wa idara, Waziri Jafo ameeleza kuwa endapo kila mtumishi
akitimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii kero na matatizo
yanayowakabili wananchi yatabaki kuwa historia.
Waziri Jafo amewataka Wakurugenzi wa Halimashauri na
Wakuu wa Idara kuweka mipango ya uendeshaji wa masuala mbalimbali ya
kimaendeleo na kujipima wamefanikiwa kiasi gani na kama walifeli wafanyaje ili
makosa hayo yasiweze kujitokeza tena, huku akiwataka kuwa wabunifu na kutafuta
mapato nje ya bajeti ili waweze kujiendesha ipasavyo na kuleta maendeleo katika
taifa na kuwahakikishia madiwani kushughulikiwa kuhusu suala la posho na malipo
kwa watumishi.
Kwa upande wake Meya wa Halmashauri hiyo Charles
Kuyeko amepongeza jitihada zinazofanywa na Naibu Waziri huyo na kumuahaidi
wataendelea kuyafanyia kazi maagizo yake, ambapo akiyataja baadhi ya maagizo
ambayo wameyafanyia kazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Palela Nitu ameeleza
kuwa tayari wameunda Bodi mpya ya Soko la Samako Feri kufuatia maagizo yake, na
maboresho ya sehemu ya kuwahudumia wagonjwa wa kifua kikuu TB kwenye
Zahanati ya Buyuni iliyopo Chanika.
Vilevile Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es
Salaam Sipora J. Liana amemueleza Naibu Waziri Jafo katika
kuhakikisha jiji linaendelea, tayari wametekelezaji uboreshaji wa huduma ya
usafiri kwa umma ili kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo,sambamba
na uboreshaji wa huduma ya afya na mazingira.