MASHIRIKA YA ACTION AID, TGNP YAWAITA WADAU KUIJADILI SHERIA YA NDOA...WAKWEPA KUJADILI UMRI WA KUOA NA KUOLEWA
Sheria
ya Ndoa nchini Tanzania ni moja kati ya sheria ambazo zimekuwa zikizua mijadala
kwa kipindi kirefu hadi kufikia hatua ya baadhi ya wanaharakati kufungua kesi
mahakamani kupinga baadhi ya vifungu vinavyokikinzana na katiba ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Miongoni mwa vifungu ambavyo vimekuwa gumzo katika sheria ya ndoa ni kifungu nambari 13 kinachoelezeza umri wa
mwanaume kuoa, pamoja na umri wa mwamke kuolewa.
Sheria inasema mwanaume anatakiwa kuoa akifika umri wa miaka 18 huku
wanawake wanatakiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 15, jambo hilo
limelalamikiwa sana wakisema mtoto wa kike hakutendewa haki kwani naye alipaswa
kuolewa akifikisha umri wa miaka 18.
Kufuatia hali hiyo Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Action Aid na TGNP Tanzania
wamewakutanisha wadau kutoka asasi za kiraia,wanazuoni na wanahabari ili kuwapa
fursa ya kuipitia sheria hiyo na kupendekeza baadhi ya marekebisho ambayo
wanadhani yanastahili kufanyika.
Akizungumza na wadau sababu za
kuijadili sharia hiyo, Mshauri wa haki za wanawake na ardhi kutoka Shirika la
Action Aid, Bi. Scholastica Haule amesema dhamira ya kuichambua sheria hiyo ni
kutaka kupata maoni ya wadau yatakayoweza kuihuisha sheria ili iweze kuendana
na wakati wa sasa.
Amesema zoezi la kuijadili sheria
hiyo litahusisha kada zote ikiwamo viongozi wa dini ambao sheria inawagusa moja
kwa moja kwani wao wamekuwa wakifungisha ndoa kila kukicha hivyo wanazijua
changamoto wanazokumbana nazo kupitia sharia hiyo.
Bi. Haule amesema, kwa hali ilivyo ni
dhahili kunahitajika mabadiliko juu ya sharia ya sasa,ukizingatia kuwa imekuwa
ikizua migogoro katika jamii.
“Hii sheria sasa ina umri wa miaka 45
toka kutengenezwa na imekuwa ikilalamikiwa sana na wadua mbalimbali wakiwamo
wanaharakati wa haki za binadamu, na wengine kufikia hatua za kufungua kesi
mahakamani. Ni dhahili watu wameona inanyima haki kwa wengine”Alisema
Aidha kwa upande wake, Mhadhri wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha sheria Dkt Hashir Twaib Abdallah
amekili kuwa sheria ya ndoa ya mwaka
1971 ambayo pia ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002 bado inachangamoto
nyingi ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi ili sheria hiyo iweze kwenda na wakati.
Dkt Hashir amesema Ukipitia sharia
hiyo yote, utagundua inamapungufu ukiachilia vifungu vichache ambavyo vimekatiwa
rufaa mahakamani
Ameongeza kusema, makundi mbalimbali
ambayo yatapata fursa ya kuijadili na kutoa maoni yao kuhusu sharia hiyo
wanapaswa kuitendea haki fursa hiyo ili sharia itakayopatikana iweze kuwa ya
manufaa kwa miaka mingi ijayo.
“Kwanza lazima tuwe makini wakati tunaipitia
sharia hii.. ifahamike kuwa sisi ni miongoni mwa watu wachache tuliopata fursa
ya kuipitia na kuwasilisha mawazo ya wengi juu ya sharia hii ambayo inagusa
Taaasisi nyeti ya ndoa. Tuwe makini kuitengeneza sharia hii ambazo tunazani
inaweza kutumika kwa miaka mingine 45”Alisema Dkt Hashir.
Ametaja baadhi ya vifungu ambavyo
vinaonekana kuhitaji marekebisho ya haraka kuwa ni pamoja na Kifungu namba 69
(1) kipenge cha (a) na (b), kinachozungumzia habari ya kulipana fidia, kutokana
na ahadi ya ndoa kushindwa kufanyika, kifungu hiki kimeonekana kina tatizo.
Amesema Kifungu kinaonekana
hakitambui suala la gharama ambazo zimetokana na ahadi ya ndoa. Kitendo hicho
kinamnyima haki aliyetendew na kuongeza kuwa kunahaja ya kukifanyia marekebisho
ili kiendane na hali ya sasa ambayo watu wengi wamekuwa wakiingia hasara ya
kusomesha wapenzi wao na mwisho wa siku wanaachwa solemba.
Kingine ni Kifungu namba 72,
kinachozungumzia kuhusu fidia juu ya wagoni, sharia imetoa mwanya watu
kuendelea kufanya uzinzi, haikuweza kuweka adhabu kali kwa wahusika matokeo
yake tumekuwa na utitili wa nyumba za kulala wageni ambazo zimegeuzwa kuwa
nyumba za uzinzi.
Kifungu hiki kinaona suala la ugoni
ni jambo la watu wawili, halina athari yoyote katika jamii na ni vigumu
kutambua na kuzuia kosa hilo kwani limekaa katika mtindo ambao ni mtu wa tatu
hawezi kuingilia jambo kama hilo.
Hapo ndio mwanzo wa matatizo makubwa,
watu wameanza kudharauliana, mwenye fedha anamdharau mwingine akiamini kuwa
hakuna sharia inayoweza kumtia kifungoni, na kwake suala la fidia ya malipo ni
jipesi na hawezi kubabaika. Alisema.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Mwanaharakati
wa haki za binadamu na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Serikali la Msichana
Initiative, Rebecca Gyumi alifungua kesi ya kikatiba katika mahakama Kuu kanda
ya Dar es salaam Tanzana akipinga sharia ya ndoa.
Shauli
hilo namba 5 lilifunguliwa kupitia wakili Jebra Kambole ambapo walikuwa
wanaidai mahakama kufuta vifungu vya 13 na 17 ambavyo vinatoa mwanya kwa watoto
wa kike kuolewa wakiwa wadogo.
Kuja kwa mchakato wa kurekebisha sharia hiyo
sasa zinaweza kuwa habari njema kwa wadau mbalimbali ambao walikuwa wanakwazwa
na sharia ya sasa.