Zinazobamba

KINGWANGALLA AITETEA WIZARA YAKE KUHUSU KEMIKALI ZA VIWANDANI NA MAJUMBANI ,SOMA HAPO KUJUA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla akizungumza  wakati akitoa tamko kuhusu ubora wa bidhaa za vilainishi nchini. Leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mohamed Ali Mohamed


Waziri ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dkt Khamis Kigwangalla  ametangaza kuwa wizara  yake kupitia Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepewa dhamana ya kusimamia sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani ni kuhakikisha nchi inalindwa ili isiwe soko la bidhaa hafifu.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na watoto,  Dkt Kigwangalla amesema kuwa sheria hiyo pia itasaidia kuchunguza vilainishi pamoja na Kemikali zinazoingia na kutumika nchini ziwe zenye kukidhi ubora na salama katika kulinda afya na mazingira ya Taifa letu. 

"Katika karne hii ya “Utandawazi” yenye maendeleo makubwa ya Sayansi na Teknolojia, wananchi na wawekezaji wanahitaji kuhakiki ubora na usalama wa bidhaa zao ili ziweze kukubalika katika soko la kitaifa na kimataifa".

Amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa mizigo ya bidhaa za vilainishi nchini, kumekuwepo na taarifa za uwepo wa bidhaa za vilainishi visivyo na ubora katika matumizi mbalimbali.
Aidha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto ametoa agizo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuaendelea na uchunguzi wa kimaabara wa bidhaa za vilainishi vilivyo sokoni, kwa kushirikiana na makampuni yenye nembo halisi “trade-marks” ili kubaini na kutambua bidhaa za vilainishi halisi na visivyokidhi viwango vya ubora. 

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele amesema kuwa wataendelea na uchunguzi wa kimaabara kwa kuchukua sampo kutoka sokoni ili waweze kuona vilainishi vilivyopo sokoni kama vinaendana na viwango, ambapo katika zoezi hilo pia watawapata watu ambao wanafanya biashara isiyokubalika ambao watapewa onyo na kuendelea kufanya biashara zao na ikiwa bado wataendelea sheria itafuata nkondo wake. 

Hata hivyo Serikali imepiga marufuku uuzaji wa vilainishi vya kupima unaofanyika mtaani na sokoni kwa sababu vifungashio vya vilainishi hivyo havikidhi ubora na pia bidhaa hizo zinaharibu ubora wa vilainishi na hivyo kuathiri utendaji wa mitambo inayotumia vilainishi.