HIVI NDIVYO CCM ILIVYOSUKWA UPYAA,SOMA HAPO KUJUA
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe
13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao
hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.
Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya
CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya
kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;-
1. Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya
vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa
Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma
badala ya kutumia muda mwingi vikaoni.
Ili kuwa na vikao vya Chama vyenye tija
imeamuliwa kama ifuatavyo:-
a). Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya
wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na
kuwa wajumbe 158 kama ifuatavyo:-
Wenyeviti wa Mikoa
Mikoa ya
Bara
26x1 = 26
Mikoa ya Zanzibar
6x1 = 6
Wajumbe wa NEC wa Mikoa
Mikoa ya Bara
26x1
= 26
Mikoa ya Zanzibar
6x4
= 24
Wajumbe wa NEC wa Taifa
Kutoka Bara
=
15
Kutoka Zanzibar
=
15
Nafasi za Mwenyekiti
=
7
Wajumbe wa NEC wa Jumuiya
UVCCM = 5
UWT = 5
WAZAZI = 5
Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni
= 5
Katibu wa Kamati ya Wabunge wa
CCM = 1
Wajumbe wa NEC kutoka BLW
= 3
Katibu wa Kamati ya Wawakilishi
= 1
Wajumbe wa NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao
- Mwenyekiti wa
CCM
= 1
- Makamu Mwenyekiti
(B)
= 1
-Makamu Mwenyekiti
(Z)
= 1
- Makamu wa
Rais
= 1
- Waziri
Mkuu
= 1
- Makamu wa Pili wa Rais (Z)
= 1
- Spika wa
Bunge
= 1
- Spika wa
BLW
= 1
- Mwenyekiti wa
UWT
= 1
- Mwenyekiti wa
WAZAZI
= 1
-Mwenyekiti wa
UVCCM
= 1
- Katibu Mkuu –
WAZAZI
= 1
- Katibu Mkuu –
UWT
= 1
- Katibu Mkuu –
UVCCM
= 1
Jumla: 158
#. Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa
vifanyike kila baada ya miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa
isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.
b). Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati
Kuu wawe 24 badala ya 34 kama ifuatavyo:-
Mwenyekiti wa CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Zanzibar)
Makamu wa Rais
Katibu Mkuu wa CCM
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Waziri Mkuu
Makamu wa Pili wa Rais (Z)
Spika wa Bunge la Tanzania
Spika wa BWL
Mwenyekiti wa WAZAZI
Mwenyekiti wa UWT
Mwenyekiti wa UVCCM
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa
wa Organaizesheni
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa
wa Itikadi na Uenezi
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa
wa Uchumi na Fedha
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa
wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa
na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania
Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na
Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar.
#. Vikao vya kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili
vifanyike kila baada ya miezi minne badala ya miezi miwili isipokuwa
vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.
c). Kwa ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za
Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa wajumbe watatu ambao ni:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa
Mkoa
- 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na
H/Mkoa
- 2
#. Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya
Mkoa vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi kama
ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.
d). Kwa upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa
ya Wilaya wapunguzwe kwa kuwoandoa:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa
Wilaya - 1
Katibu wa Kamati ya
Madiwani
- 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)-
2
Jumla: 4
#.Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa
ya Wilaya vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi
isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.
#. Muundo wa Wilaya za Chama uendane na muundo wa
sasa wa Serikali.
Kata,Tawi na Shina
Idadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50 hadi
300.
Idadi ya kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301
hadi 1,000.
Hata hivyo idadi hii izingatie eneo la kijiografia
na wingi wa wanachama katika eneo hilo.
Vikao vya kawaida vya Kamati za Siasa
za ngazi hizi viwe vinafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu,
isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.
#. Nafasi za Uongozi
Mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya
uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa
Chama Toleo la 2012 kifungu cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:-
Mwenyekiti wa Tawi,Kijiji au Mitaa.
Mwenyekiti wa Kata/Wadi.
Mwenyekiti wa Jimbo, Wilaya na Mkoa.
Makatibu wa Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika.
Mbunge, Mwakilishi na Diwani.
#. Viongozi wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji
badala yake waongoze na kusimamia shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na
Kanuni.
#.Vyeo ambavyo haviko kwenye Katiba
Vyeo ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM
haviruhusiwi katika Chama au Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali
kama Wenyeviti wa ngazi mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k),
Makamanda (UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote.
#. Uhakiki wa Wanachama wa CCM
Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki
wa wanachama wa CCM na Jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama
wetu kwa wakati huu. Uhakiki huu uendane na kutoa kadi mpya za
uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na
kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki
na kadi za CCM tu.
#. Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi
Jumuiya za CCM zimetakiwa kufanya kazi zake
kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za
Jumuiya ziendane na matakwa ya Katiba ya CCM.
#.Uaendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya za
Chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la
Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi).
Makatibu Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na
Kamati Kuu na Manaibu Katibu Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya
Halmashauri Kuu ya Taifa.
#. Wakati tukiendelea kubaki na Bendera yenye
rangi ya kijani na njano na alama ya jembe na nyundo, Halmashauri
Kuu imeona ipo haja ya kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi.
#. Utumishi katika Chama na Jumuiya
zake. Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za
Watumishi wa Chama na Jumuiya zake.
Nafasi za Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya
zitaondolewa na badala yake kazi zao zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya
za Chama wa Mikoa na Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa. Utaratibu huu
utakipunguzia Chama Cha Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa
Chama na Jumuiya zake katika Mikoa na Wilaya.
#. Tathimini ya hali ya Kisiasa na Uchaguzi
wa Zanzibar .
Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kuundwa kwa Kamati
maalum ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla
na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar 2015.
# Mwenyekiti wa Kamati ya udhibiti na nidhamu
ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka
mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari
2017, Mikoa na Wilaya ambazo hazijaleta taarifa zao za kiudhibiti ziwe
zimefikisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti na Nidhamu kabla
ya tarehe 30/01/2017.
#. Uhakiki wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa
kina na uchambuzi zaidi ukikamilika Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti
ya Halmashauri Kuu ya Taifa mapema iwezekanavyo.
#. Maamuzi na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika
kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na Kanuni za Jumuiya za Chama.
#. Kwa mambo yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya
Katiba, Mkutano Mkuu utaandaliwa mapema mwakani na kutafakari na kupitisha
mabadiliko hayo ya Katiba.
Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti
ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu
mengine ya kiserikali.
#.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye
ameteuliwa kuwa balozi.
#. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro
aliyeteuliwa kuwa Balozi
#. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa
Waziri.
#. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.
Imetolewa na:-
NAPE NNAUYE
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
13/12/2016