HATIMAYE MMILIKI WA JAMIIFORUM APATA DHAMANA,SOMA HAPO KUJUA
Mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums Maxence
Melo ameachiwa kwa dhamana leo katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, baada ya kukaa mahabusu kwa takribani siku 5.
Melo anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la
kumiliki na kuendesha tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini Tanzania
(JamiiForums).
Mashtaka mengine ni kuzuia na kuharibu taarifa
ambazo Jeshi la Polisi wamekuwa wakizitaka kwa ajili ya uchagunguzi chini ya
kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Mitandao na kushindwa kutoa ushirikiano
kwa Jeshi la Polisi na kuharibu uchunguzi chini ya kifungu cha namba 22
cha Sheria ya Makosa ya Mitandao.